JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA
Simu Na: (026) 2322848, 2321607,
2322853, 2322420,
Nukushi: (026) 2322116, 2322146.
2321013,
|
|
Tawala
za Mikoa
na
Serikali za Mitaa,
S. L. P.
1923, DODOMA.
|
TAARIFA
KWA UMMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya
Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma
Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D.
Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha
urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.
Kutokana na hali hiyo Mhe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na
Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi
dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.
Agizo hili limetolewa na
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi
kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Katika uchunguzi ambao umefanyika
katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi
ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali
hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.
Aidha, Mhe. Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini
kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate
leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.
Mhe. Simbachawene ametoa
agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha
na vitendo vya rushwa.
Imetolewa
na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais - TAMISEMI
30 Desemba, 2015
No comments:
Post a Comment