Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (wa pili
kulia) mara baada ya kuwasili Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza
kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Prof. Adolph Mkenda akifafanua jambo
ofisini kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango mara baada ya kuwasili
Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa fupi kwa
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia) ikiwa ni sehemu
ya ukaribisho kwa Waziri huyo Wizarani hapo.
Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakielezea majukumu ya Idara
na Vitengo katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip mara
baada ya kuwasili Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kadi aliyoipokea
kutoka kwa viongozi kwaniaba ya watumishi wa Wizara hiyo yenye lengo la
kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Wa kwanza kulia ni Kaibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mkurugenzi Idara ya
Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Deodatha Makani (katikati).
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
Watumishi Wizara ya Fedha na Mipango wameaswa
kufanya kazi kwa weledi na kuwekeza
nguvu zaidi katika ukusanyaji mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi
iwe kitovu cha uchumi Barani Afrika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo alipowasili
Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Katika
mazungumzo yake na watendaji hao, Mhe. Dkt. Mpango, aliuagiza uongozi wa Wizara yake kuunda na kisimamia sera za mfumo wa ukusanyaji kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa
wafanyabiashara ili kukuza biashara na uwekezaji nchini.
“Ili kutekeleza kutekeleza ukusanyaji
wa kodi kwa kutumia mfumo rafiki kwa wafanyabiashara na Serikali, Wizara
inawajibu wa kusimamia na kukuza uchumi ambao utawanufaisha wananchi walio
wengi, kwa kuhakikisha kodi zote ndogondogo ambazo ziko chini na nje ya Wizara,
ambazo ni kero kwa wanachi wa hali ya chini zinapatiwa ufumbuzi kwani wananchi
hao nao wanastahili maisha mazuri” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Waziri Dkt. Mpango aliwasisitiza watendaji
kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi ili nchi iweze kupiga hatua kwa
kuzingatia nidhamu katika kufanya kazi ambayo ni dhamana walizokabidhiwa.
Naye Naibu Waziri Wizara ya Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahimiza watendaji wa wizara hiyo kufanyakazi
kwa umoja na mshikamano waliokuwa nao katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo
yenye tija huku akisisitiza kuwa wizara hiyo ndiyo msingi katika kukuza uchumi wa
nchi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile aliwapongeza
Viongozi hao wapya wa Wizara kwa kuteuliwa kwao kuiongoza Wizara ambayo ndiyo
muhimili wa Serikali.
Aidha, Dkt. Likwelile alitoa wito kwa
watendaji wa wizara hiyo kuzingatia maagizo ya Mhe. Waziri kwa maendeleo ya
nchi ili kulinda hadhi na heshima ya wizara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Fedha na Mipango
28 Desemba, 2015
No comments:
Post a Comment