Naibu mkuu wa Rasilmali Watu nwa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Doris Luvanda akipokea kikombe cha mshindi wa mwajiri bora wa mwaka 2015 kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kuhitimisha hafla hiyo. Kulia ni Katibu mkuu Dkt Florens Turuka na mwenyekiti wa ATE Almas Maige, Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Meck Sadiki na Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka.
Dar Es Salaam,
Maadili ya kazi yanayoonyeshwa na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya
mikononi ya Tigo Tanzania pamoja na juhudi zinazohitajika katika nyanja ya
mawasiliano ya simu ulionyeshwa kuwa mfano katika tuzo mbalimbali
zilizonyakuliwa na kampunin ya Tigo Tanzania.
Haya yalijidhihirisha
katika sherehe ya kuizawadia kampuni ya Tigo wakati wa sherehe ya mwaka
ya utoaji tuzo ya mwajiri bora wa mwaka unaoendeshwana chama cha waajiri
Tanzania (ATE) zilizofanyika Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya
kupokea tuzo hiyo, Meneja Rasilimali Watu wa kampuni ya Tigo, Doris Luvanda
alisema : “tumekuwa tukifanya kazi kwa kasi kadri ambavyo sekta ya rasilimali
watu ilivyo kwa sasa na tumehakikisha ya kuwa waajiriwa wetu wamefahamishwa
kikamilifu kuhusu bidhaa zetu, na mafunzo ya ndani kila siku yametujengea
uimara kwa waajiri wetu
Tigo imefaulu kushinda
nafasi za ushindi mbalimbali kama vile Sera ya ujumla ya rasilimali watu na
ulinzi, malipo na faida zake.
“Maandalizi ya mashindano
yanatayarishwa na mshauri wa kujitegemea anayefanya kazi kuhakikisha ya kuwa
chama cha waajiri Tanzania (ATE) kinampata mshindi halali ambaye
hujulikana mara tuu baada ya kupitia yale yaliyowasilishwa kwa ajili ya
ushindani kukamilika, Mkurugenzi wa ATE, Dr. Aggrey Mlimuka alisema.
Kufuatia mapokezi
mazuri ya kila mwaka kwa ajili ya shindano hili la mwaka, kwa mwaka huu jumla
ya makampuni 135 zilijaza masuali ya kuandika na baadhi yao 63 zilifanikisha
kushiriki kikamilifu katika shindanoahili.
No comments:
Post a Comment