Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
akimzungumza na watumishi wa Serikali na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika
Ukumbi wa NSSF mjini humo. Majaliwa aliwataka watumishi wa mkoa huo wafanye
kazi kwa juhudi ili kuuletea maendeleo zaidi mkoa huo. Waziri Mkuu
Majaliwa, pia aliwaonya wakimbizi wa
Kambi ya Nyarugusu na Nduta kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa
usalama katika kambi hizo . Kulia meza kuu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
akimkabidhi mkimbizi Cesiwa Angelani (kushoto) zawadi ya ndoo yenye vifaa vya
kumuhudumia mtoto baada ya mzazi huyo kujifungua katika Hopsitali iliyopo
katika ya Nyarugusu ambapo Wakimbizi wanahifadhiwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza
na wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu (hawapo pichani) wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma,
wakati alipofanya ziara ya kutembelea kambi za wakimbizi mkoani humo. Majaliwa
aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama
katika eneo waliohifadhiwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga.
Sehemu ya Wakimbizi wa Kambi ya Nduta,
Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa (hayupo pichani) wakati alipokuwa
akizungumza na wakimbizi hao. Majaliwa aliwaonya wakimbizi hiyo kutojihusisha
na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika kambi hiyo.
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Kambi
ya Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara katika kambi
hiyo. Katika hotuba yakekwa wakimbizi wa kambi hiyo, Majaliwa aliwaonya
wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika
eneo waliohifadhiwa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akimwagilia mti wa kumbukumbu
alioupanda katika Kambi ya Nduta, Wilaya
ya Kibondo mkoani Kigoma wakati Waziri huyo alipoambatana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
katika ziara katika kambi hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa aliwaonya
wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama katika
eneo waliohifadhiwa.
Mkuu
wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, wilayani Kibondo, Fred Nsijile akitoa taarifa
ya kambi yake kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto). Katika
taarifa hiyo Mkuu wa Kambi alisema kambi yake inakabiliwa na upungufu wa maji
kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoishi kambini humo. Hata hivyo katika
hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa alisema atalifanyia kazi tatizo hilo na pia aliwaonya
wakimbizi katika kambi hiyo kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa
usalama katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kushoto meza kuu ni Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Job Masima (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,
Harrison Mseke.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia)
akiwafurahia wacheza ngoma ambao ni
wakimbizi kutoka Burundi wakati walipokuwa wanamkaribisha katika Kambi ya Nduta,
mkoani Kigoma kuzungumza na wakimbizi hao. Katika hotuba yake, Majaliwa
aliwaonya wakimbizi hao kutojihusisha na uhalifu ili waweze kuishi kwa usalama
katika eneo waliohifadhiwa. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment