Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt.
Leonard Chamuriho akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa
kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa
Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa
kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Na Frank Mvungi -
Maelezo
Baraza
la Taifa la Ujenzi limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi
katika kipindi cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi
nchini.
Hayo
yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard
Chamuriho wakati wa mkutano na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Akizungumzia
majukumu ya Baraza hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta hiyo,
Mhandisi Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea
Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi, Ubora wa kazi, uelewa wa vipengele
mbalimbali vya mkataba katika mradi husika na moja ya pande zinazohusika kukatisha
mkataba.
Kakika
kukabiliana na migogoro hiyo, Baraza hilo limekuwa likitumia njia mbalimbali
ikiwemo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa pande zinazohusika katika mradi, kuwakutanisha
wadau chini ya Baraza, kuweka wahusika chini ya aliyetatua mgogoro husika.
Akifafanua,
Mhandisi Dkt. Chamuriho amebainisha kuwa Baraza hilo limekuwa likitumia njia
hizo kutatua Migogoro katika sekta hiyo pale inaposhindikana wahusika wanaweza
kwenda mahakamani kama hatua ya mwisho
katika kutatua mgogoro husika.
Pia
alitoa wito kwa watanzania wote hasa wadau wa Sekta ya Ujenzi kuwa na uelewa
mzuri wa jinsi ya kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia Sheria na kanuni
ili kuepuka Migogoro.
Baraza
la Taifa la Ujenzi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya
Bunge namba 20 ya mwaka 1987 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008.(National
Construction Council Act, CAP 162,R.E.2008) ambapo Baraza lilianza kufanya kazi
tarehe 17 August 1981.
No comments:
Post a Comment