Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akimsikiliza
aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali
ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini
Dar es salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akipokea
taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya
Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati
wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa
Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya
Nne Dkt. Seif Rashid (kushoto) akisalimiana na Naibu waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangala (kulia) leo jijini Dar
es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amekabidhiwa
rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa
Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid leo jijini Dar es salaam.
Akipokea
ofisi hiyo, Waziri Ummy alimshukuru Dkt. Seif kwa jitihada kubwa waliyofanya ya
kupambana na magonjwa kwa wananchi na kufanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa
nchi duniani ambayo imetatua tatizo la ugonjwa wa polio na kuwa “polio free”.
Aidha,
Waziri Ummy amemhakikishia Dkt Seif kuendelea kushirikiana naye pale msaada
wake utakapohitajika kwa kuwa anauzoefu katika masuala ya afya ili kuwahudumia
Watanzania na kupambana na adui wa taifa ambaye ni magonjwa.
Akikabidhi
ofisi, Dkt Seif aliwapongeza Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamisi
Kigwangalla kwa kupewa nyadhifa hizo na kuahidi kuwapa ushirikiano wake
paleutakapohitajika.
Dhana
ya “Hapa Kazi Tu” imechukua mkondo wake ambapo hadi sasa Mwaziri na Manaibu
waziri wanatekeleza dhana hiyo kwa vitendo na siyo kukaa ofisini, kwa kwa
juhudi hizo viongozi kwa kushirikiana na wananchi, Tanzania itafanikiwa kufikia
uchumi wa kati ifikapo 2025 ikiwa na watu wenye afya bora inayowaruhusu
kufanyakazi kwa juhudi na maarifa ili kuwa maendeleo yenye tija kwa Wtanzania.
No comments:
Post a Comment