Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 29 December 2015

TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK



Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa Facebook, www.facebook.com/TigoTanzania  kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa Tanzania.

Kutokana na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapa nchini, Facebook imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutokana uzinduzi wa Facebook katika lugha ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na Facebook, ambapo wateja wanaweza  kutumia  Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada.

 Ukurasa wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za  kampuni.

Hivi karibuni, Tigo Tanzania imejishindia   tuzo mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambayo inatambua mashirikana watu binafsi katika uongozi. Tuzo hizo ni ya Ubora wa  bidhaa (The Hall of Fame in Brand Excellence), na Matumizi Bora yaMitandao ya  Kijamii KatikaMauzo    ( Best use of Social Media in Marketing).

Tigo Tanzania inaongoza katika soko la mawasiliano na imekuwa mstari wa mbele katika mitandao ya kijamii ambapo wateja wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa haraka.
Hii imeufanya mtandao kuaminika sana na wateja na kutumika kama mwendelezo wa huduma kwa  wateja.

Kuhusu Facebook Mkurugenzi wa Tigo Bwana Diego Gutierrez anasema. “Jukwaaletula Facebook na Twitter (Tigo TZ) limekuwa kitendea kazi muhimu ambacho kinatumika kujifunza kutoka kwa wateja wetu na jamii kwa jumla ambao wanakitumia. Tunajivunia kwakuweza kuyafikia mafanikio haya, na tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa na  imani nasi.


Tigo,imedhamiria kubadilisha mtindo wa maisha wa kidijitali  kwa kuwaletea wateja wetu ubunifu wa teknolojia maridhawa. Hivikaribuni, tumezindua teknolojia ya 4G LTE hapa Tanzania ambayo ni intaneti iliyo na kasi kuliko zote pamoja na ofa ya aina ya simu yaTechno Y3 Smartphone inayotumia lugha ya Kiswahili.

No comments:

Post a Comment