Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimuaga kwa kumpungia
mkono Naibu Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China,
Wang Jiang (kushoto ndani ya gari) wakati kiongozi huyo wa China akiwa
anaondoka mara baada ya kumaliza ziara yake nchini. Juzi Waziri Kitwanga na
Naibu waziri huyo wa China walisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika
masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa Raia kati ya Wizara hizo mbili,
katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar
es Salaam. Kulia kwa Waziri Kitwanga ni Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi,
Kamishna Thobias Andengenye. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang
(kushoto) akimshukuru kwa kukaribishwa vizuri nchini pamoja na ushirikiano waliofanya
baada ya kusaini kusaini Hati ya
Makubaliano mwanzoni mwa wiki hii katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Naibu
Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang
(kushoto) wakati alipomsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga kiongozi huyo wa China. Naibu Waziri
huyo wa China na Waziri Kitwanga, mwanzoni mwa wiki hii walisaini Hati ya
Makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara hizo mbili. Kulia ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil. Picha na Kitengo
cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akifurahi jambo na Naibu
Waziri wa Wizara ya Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Jiang
(kushoto) wakati walipokuwa wanaagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.. Naibu Waziri huyo wa China na Waziri
Kitwanga, mwanzoni mwa wiki hii walisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano
kati ya wizara hizo mbili. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
No comments:
Post a Comment