Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la
Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) wakati
alipokitembelea kituo hicho cha Polisi jijini Dar es Salaam leo. Pia Waziri
Kitwanga katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza wizara
hiyo, alitembelea Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), pamoja na
kukagua nyumba za Makazi ya Polisi za sasa na zamani zilizopo barabara ya Kilwa.
Wanne kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha zote
na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akitoka kuikagua moja ya nyumba ya zamani ya
Jeshi ya Polisi ambayo inakaliwa na baadhi ya askari iliyopo Barabara ya Kilwa
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Waziri Kitwanga alizikagua nyumba hizo za zamani pamoja na zakisasa zilizopo
katika eneo hilo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiiangalia nyumba ya mabati ya makazi ya Polisi
wakati alipoingia ndani huku akitokwa na jasho kutokana na joto kali ndani ya
nyumba hiyo. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kutembelea nyumba hizo zilizopo
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na kushoto ni mkazi wa nyumba hiyo, ambaye ni askari
Polisi, Nelson Chale. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil (kushoto) wakizikagua nyumba za kisasa ambazo ni za ghorofa za Jeshi
ya Polisi nchini zilizopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri
Kitwanga alifanya ziara kuzitembelea nyumba hizo ili kujionea ukosefu wa nyumba
unaowakabili Polisi nchini. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi,
Kamishina Thobias Andengenye (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar
es Salaam (DPA), DCP Ally Lugendo (wapili kulia) wakikwepa waya wakati
walipokuwa wanamuonyesha Waziri Kitwanga mabweni ya Chuo hicho kilichopo
barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga akilikagua moja ya darasa linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo
cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA). Waziri Kitwanga alifanya ziara ya
kukitembelea chuo hicho pamoja na kuzungumza na wakufunzi wa chuo hicho. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akionyeshwa moja ya gari la maji washa, na
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova katika Kambi
ya Jeshi la Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri
Kitwanga alifanya ziara kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akiwauliza maswali Mkuu wa Utawala wa Jeshi
la Polisi, Kamishina Thobias Andengenye (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Taaluma
ya Polisi Dar es Salaam (DPA), DCP Ally Lugendo wakati Waziri huyo alipofanya
ziara katika Chuo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri
Kitwanga alifanya ziara hiyo ili ajifunze mambo mbalimbali yanayofanywa na
Jeshi la Polisi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akimsikiliza kwa makini Mkufunzi wa Chuo cha
Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Inspekta Novatus Akondowe (kulia) alipokuwa
anamuuliza swali. Waziri Kitwanga alitoa ruhusa ya kila mkufunzi wa chuo hilo
waeleze matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo chuoni hapo. Picha na Kitengo
cha Mawasiliano-MOHA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari
alioambatana nao wakati wa ziara yake katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo
jijini Dar es Salaam. Pia Waziri huyo katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu
alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, alitembelea nyumba ya Makazi ya Polisi
barabara ya Kilwa, Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kituo cha Polisi Msimbazi
na Kituo cha Polisi Oysterbay. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
No comments:
Post a Comment