
Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Akizungumzia maandalizi ya shoo hiyo, Diamond alisema itakuwa ya tofauti. Kila atakayelipia fedha yake ( kawaida shilingi 15,000 na V.I.P shilingi 30,000) hatojutia.
"Tukutane pale Dar Live, tuimbe na kucheza nyimbo zote za Diamond kuanzia Kamwambie, Lala Salama, Moyo Wangu, Mbagala, Nimpende Nani, Nitarejea, Ukimuona, Nataka Kulewa, Kesho, Nasema Nao, Mawazo, Number One, Nana, Nitampata Wapi, Kizaizai, MdogoMdogo, BamBam na Utanipenda ambao ndiyo habari ya mjini kwa sasa," alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment