Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi
Kigwangalla akiwa amekwisha amuru geti kungwa mara baada ya saa 1:30 asubuhi
ambao ndiyo muda wa mwisho wa watumishi kufika kazini ili kusimamia suala la
nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini
Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisaini moja ya vitabu vya mahudhurio ya wafanyakazi katika Wizara
hiyo mara baada ya saa 1:30 asubuhi ambao ndiyo muda wa mwisho wa watumishi
kufika kazini ili kusimamia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini
kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi
Kigwangalla (kushoto) akiongea na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw.
Michael John (kulia) kujua utaratibu mzima wa watumishi kufika kazini ambapo
Naibu Waziri huyo amefuatilia kwa wiki nzima na kubaini kuwepo uchelewaji
kazini mara baada ya kuamuru geti kungwa mara baada ya saa 1:30 asubuhi ambao
ndiyo muda wa mwisho wa watumishi kufika kazini ili kusimamia suala la nidhamu
ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es
salaam.
Moja ya Daftari ya mahudhurio ya wafanyakazi ambayo imesainiwa tayari na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi
Kigwangalla jana jijini Dar es salaam.
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
Wafanyakazi Wizara wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee wametakiwa kuzingatia suala
la muda wa kufanyakazi kuanzia kuingia kazini hadi muda wa kutoka baada ya muda
uliopangwa.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi
Kigwangalla alipokuwa akifuatilia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi
kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.
“Wafanyakazi wanawajibu
wa kuwahi kazini saa 1:30 asubuhi kama ilivyopangwa kwa mujibu wa taratibu za
utumishi wa umma na kutoka saa 9:30 baada ya muda wa kazi, hatuwezi kuendelea
kuvumilia tabia ya watu kuendelea kumwibia mwajiri muda wa kufanyakazi”,
“Sisi tumewahi kazini,
Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na viongozi wengine, halafu watumishi
wanachelewa, tumeonesha mfano, tunawahi na tunachelewa kuondoka” akisema Dkt.
Kigwangalla.
Kwa mujibu wa taratibu
za kazi, ilipofika saa 1:30 asubuhi, Dkt. Kigwangalla aliamuru walinzi kufunga
geti na kutoruhusu waliyechelewa kuingia hadi atakapo maliza kusaini madaftari
ya mahudhurio kulingana na idara na vitengo vilivyopo waizarani hapo.
Idara hizo ni pamoja na
Utawala, Kinga, Mafunzo, Tiba, Udhibiti na Uhakiki Ubora, Mganga Mkuu, Uhasibu,
Sera na Mipango, Wauguzi na Famasia pamoja na vitengo vya Sheria, Mawasilano
Serikalini na Tehama.
Akisisitiza Dkt.
Kigwangalla alisema kuwa wanachokifanya ni kuahakikisha zoezi la kukomesha
tabia ya uchelewaji linakuwa endelevu kwasababu watumishi wameajiriwa ili
kuwahudumia wananchi, ufuatiliaji huo utakomesha tabia ya watumishi kuchelewa
kufika kazini na kuondoka mapema kabla ya muda wakazi.
Vilevile Dkt. Kigwangalla
alisema kuwa watumishi wafanye kazi kwa kujitolea, maana Tanzania itajengwa na
zama za kazi ambapo wao viongozi wamewapa watumishi mfano wa kuwahi kazini.
Kuhusu watumishi
waliochelewa Dkt. Kigwangalla ameagiza waandike barua za kujieleza ni kwake na
azipate jana hiyo hiyo ambapo zoezi hilo la amemkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu Bw. Michael John.
Aidha, katika kudhibiti
tabia ya uchelewaji, Dkt. Kigwangalla amemwagiza Bw. Michael ammueleze kwa
maadishi ni kwanini Wizara hiyo haijachukua hatua ya kuingia katika mfumo wa
dijiti (Biometric) wa watumishi kuweka vidole au kutumia kadi wakati wa kuingia
kazini ili mfumo mzima wa ofisi ujue mtumishi fulani amefika kazini saa ngapi
na kama atatoka ajulikane yupo wapi na kwa nini.
Dkt. Kigwangalla amesema
kuwa amefikia hatua hiyo ya kusimamia kukomesha tabia ya uchelewaji kutokana na
Wizara hiyo kulaumiwa kwa na urasimu, kumbe watumishi hawawahi kazini ambapo
yeye mwenyewe amejionea nia watu wangapi wameahi kazini.
Zaidi ya hayo, Dkt.
Kigwangalla ameagiza kupewa maelezo ya kina juu ya watumishi wa afya nchi nzima
kuanzia Madaktari, Wauguzi, Wafamasia ili aweze kujua kuna mfumo gani wa
kuangalia watumishi wamefika ofisini na wanafanya kazi ipasavyo.
No comments:
Post a Comment