Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi alipofanya ziara ya
kujua utendaji wa mamlaka hiyo, Dar es Salaam.
Akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na viongozi wa wa Ewura, Profesa Mbarawa ameagiza mamalka hiyo, kufungua haraka matawi katika Kanda mbalimbali nchini ili kurahisisha uboreshaji wa huduma za maji.
Pia ameitaka Ewura, kutoa adhabu kali kwa taasisi,mamlaka za maji na wafanyabishara wa maji wanaotoa huduma zisizoridhisha hasa kuuza maji machafu.
Waziri Profesa Mbarawa, ameuagiza uongozi wa Ewura, kumpelekea mikataba ya utendaji ya Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu, ili kila mmoja afuatiliwe uwajibikaji wake.
Waziri, Profesa Mbarawa ambaye katika ziara hiyo alifuatana na Naibu wa Wizara hiyo, Injinia Isack Kamwela, amesifia utendaji mzuri wa mamlaka hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:
Post a Comment