Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya wakifatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Abbasi Kandoro. |
Wadau wakifuatilia mkutano |
Mhandisi toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya ( TCRA( Asajile Mwakisisile akitoa maada katika semina hiyo. |
Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia katika semina . |
Washiriki wa semina hiyo ya Uhamasishaji na uelimisha wa huduma za Mawasilino wakifuatilia kwa Makini semina hiyo. |
Picha ya pamoja na Meza Kuu. |
Na
EmanuelMadafa, Mbeya (jamiimojablogu )
Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Abbas Kandoro ameyaasa Makampuni ya huduma za Mawasiliano ya Simu Nchini kuhakikisha
yanaboresha huduma zao kwa kuhakikisha yanaondoa kero zote anazo kutana nazo mtumiaji wa mawasilino hayo.
Amesema moja
ya changamoto inayowakwaza watumaiji wa mawasilino hayo ni pamoja na kuweka
matangazo ya simu (Miito ya simu)ambapo hukatwa kiasi cha pesa pasipo
makubalino.
Mkuu huyo wa
Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametoa kauli hiyo jijini Mbeya wakati
akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyondesha na
Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasilino TCRA-CCC katika ukumbi
wa Mkapa jijini humo.
Amesema pamoja na kutambua mchango wa makampuni yanayotoa
huduma hizo za mawasiliano katika kuleta maendeleo ,nivyema makampuni hayo yakahakikisha
yanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu unaonekana na thamani inayolipwa na
watumiaji wa huduma hizo sanjali na kutimiza majukumu yao kwa watumiaji kama
yalivyo ainishwa katika sheria na kanuni za leseni.
Aidha Mkuu
huyo wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumiaji huduma hizo za mawasiliano ya simu
kujikita katika matumizi bora ya mitandao ya simu badala ya kujingiza katika
matumizi yasiyo sahihi ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiwango kikubwa kuondoa
maadili katika jamii pamoja na uchochezi.
Amesema kuwa sheria ya
makosa ya mitandao nchini namba 14 inaweka wazi juu ya adhabu atakayo weza kutolewa
dhidi ya mtu au kikundi kitakacho husika
na upotoshwaji wa aina yoyote .
Amesema sheria ya makosa ya mitandao inaanisha makosa na
adhabu zinazohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na teknolojia ya habari
na mawasilino.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa mbeya ametumia fursa hiyo
kulitaka baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA-
TCCC kuendelea kuhamasisha ,kuelimisha pamoja na kutambua na
kuelewa kero na matalajio ya watumiaji
wa huduma za mawasiliano nchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa
huduma za mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo ametoa wito kwa Makampuni yote
yaliyojikita katika uwekezaji wa mawasiliano ya simu ,huduma za utangazaji na
huduma za posta kuhakikisha wanaendelea kujenga mitandao ya huduma zao nchi
nzima ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo ameviomba vyombo vya habari nchini
kusaidia kulitangaza Baraza hilo na shughuli zake ili wananchi wajue ni wapi pa
kupata ushauri na kutatua matatizo yao yanayohusiana na huduma za mawasiliano.
Katika semina hiyo pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji Baraza
pia limeunda kamati ya watumiaji wa
huduma za mawasililiano kwa mkoa wa mbeya ambapo wajumbe wa kamati hiyo
walichaguliwa kutoka miongoni mwa wanasemina ambapo majukumu yao yatakuwa ni
kuelimishajamii juu ya haki wajibu na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko
sanjali na kupokea toka kwa watumiaji na kuyawasilisha kwa baraza.
No comments:
Post a Comment