Rais
Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha Charles Kitwanga (Mb) Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimpongeza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu
jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Waziri
Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es
Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta jambo na Katibu
Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, John
Mngodo mara baada ya kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya Ukumbi wa Mikutano
Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia) akimkaribisha
wizarani Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya
kuapishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha Waziri mpya wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya waziri huyo iliyopo
Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni
kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya
ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix
Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto) akimfafanulia Waziri mpya
wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli mbalimbali zinazofanywa na
wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya
Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala
mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar
es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil,
anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP), Abdurahman
Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja
(hayupo pichani). Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
No comments:
Post a Comment