Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisalimiana na
Uongozi wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji pamoja na Maofisa wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji wakati alipowasili Chuoni hapo kufunga mafunzo ya Sajini na Askari
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kozi ya Awali
yaliyofanyika hayo Chuoni hapo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akikagua Gwaride
la Heshima lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Sajini na Askari
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyofanyika katika Chuo cha yaliyofanyika
katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam.
Gwaride
la Wahitimu wa Mafunzo yaKozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji likipita mbele ya mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji
jijini Dar es Salaam.
Muhitimu
wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Semeni Daudi Chiunda, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, kutokana na kuwa Mhitimu Bora
katika kipingere cha Ukakamavu wakati wote wa Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo
cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment