Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa
KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfadhili wa chama hicho, Sanito Samson na mkewe, Dativa Sanito, wamehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakielezea kuchoshwa kuchangishwa fedha au mali ambazo zinawanufaisha viongozi wa CCM.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (Bavicha) Jimbo la Muleba Kaskazini, Robert Rwegasira, alisema Sanito na mkewe walijiunga CHADEMA katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Muyenje, Kata ya Kagoma Machi 4, mwaka huu.
“CHADEMA juzi ilifanya mkutano katika Kijiji cha Muyenje, Kata ya Kagoma, Jimbo la Muleba Kaskazini, Wilaya ya Muleba. Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana wa watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM katika jimbo hili, Sanito Samson na mkewe walipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA,” alisema Rwegasira.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment