MWENYEKITI wa muda wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho, ameonyesha kukata tamaa na kasi ya Bunge hilo inavyoenda taratibu kinyume cha matarajio.
Akizungumza kupitia kituo cha Radio One cha jijini Dar es Salaam, Kificho ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, alikiri kwamba Bunge hilo limekuwa likienda polepole pasipo kuzingatia muda.
Kificho alitoa sababu zinazochangia Bunge hilo kutokwenda kwa kasi iliyotarajiwa kwamba imetokana na wajumbe kufanya kazi bila kuwa na kanuni inayowaongoza.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment