Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 7 March 2014

CCM WADAIWA KUMCHAPA PADRI KALENGA


KAMPENI za ubunge katika Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa zimeingia katika hatua mbaya baada ya Padri wa Kanisa la Orthodox  katika Kijiji cha Nyamihuu, Kata ya Nzihi, jimboni humo Constantino Mbilinyi (36), kupigwa na watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tukio la kupigwa kwa Padri Mbilinyi lilitokea juzi baada ya kuwafikisha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kitongoji cha Igangimali walichokwenda kuweka mabango ya mgombea wao, Grace Tendega na kutangaza mkutano wa kampeni ambao ulifanyika jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, padri huyo alisema alipatwa na mkasa huo baada ya kukutana na viongozi wa CHADEMA na kumuomba awapeleke katika Kijiji cha Igangimali.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment