Huyu mwingine akiwa hoi kwa njaa na ugonjwa.
Wamepewa maji, walau nyuso zimeanza kukunjuka.
Hii ndiyo Canter iliyokuwa imewabeba.
Yanaonekana matenga ya nyanya, lakini katikati ndimo walimokuwa wamefichwa.
Gari inamilikiwa na Zuberi Kitojo, mkazi wa Tanga.
Inavyoonekana kwa mbele gari hiyo.
RPC Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari.
Na Daniel Mbega, Iringa
JESHI la Polisi mkoani Iringa limewakamata wahamiaji haramu
46 kutoka Ethiopia wakiwa njiani kuelekea Afrika Kusini.
Akizungumza na wanahabari mjini humo, Kamanda wa Polisi
mkoani Iringa, ACP Ramadhani Mungi, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa
9:50 alfajiri ya leo katika eneo la Sheli ya zamani kwenye kitongoji cha Geza
Ulole, Kijiji cha Ruaha Mbuyuni, Tarafa ya Mahenge wilayani Kilolo.
Kamanda Mungi amesema askari polisi wakiwa kwenye doria
waliwakamata wahamiaji hao haramu 46 kutoka Ethiopia wakiwa kwenye gari lenye
namba za usajili T342AJU aina ya Canter likiendeshwa na Mbega Ally (37), kabila
Mbondei na mkazi wa Tanga wakiwa wanaelekea Afrika Kusini. Dereva wa gari hilo
amekamatwa.
“Tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji hawa haramu baada ya
kupata taarifa za kiitelijensia, hii inaonyesha namna gani tulivyojipanga
kuhakikisha tunawadhibiti wahalifu wote wakiwemo wahamiaji haramu,” alisema
Mungi.
Mungi alisema kwamba, wahamiaji hao waliwekwa katikati ya
matenga (maboksi) ya kubebea nyanya ambayo yalikuwa tu.
Wahamiaji hao haramu walikuwa wamepakiwa kwenye Canter hiyo
inayomilikiwa na Bw. Zuberi Kitojo mkazi wa Tanga, ambapo wahusika walidai
kwamba walikuwa wamepakia nyanya.
Mmoja wa wahamiaji hao haramu, Shiraom Tadeu (20), amesema
kwamba wamekimbia vita Ethiopia na kwamba walikuwa wanaelekea Malawi kwenye
makambi ya wakimbizi.
“Tumetumia siku 21 porini tukikwepa vyombo vya usalama. Tumepitia
Kenya na hatimaye kuingia Tanzania, kule hali ni mbaya sana,” alisema Tadeu na
kuongeza kwamba wameshindwa kuomba hifadhi ya ukimbizi Kenya kwa sababu hali ya
amani ni tete, lakini kwa hapa Tanzania hakuna kambi hata moja ya wakimbizi,”
alisema.
Tadeu, ambaye anaongea Kiswahili kidogo, alisema kaka yake
pia yuko kwenye kambi hizo za wakimbizi nchini Malawi na ndiye amekuwa
akiwasiliana naye tangu wanatoka Ethiopia.
No comments:
Post a Comment