CHAMA KINATOA UFAFANUZI.
1.
Chama kilianzisha zoezi lililojulikana kama M4C- Operationi Pamoja
daima(M4C-OPD), katika zoezi hili chama kilifanya mikutano zaidi ya 360
karibu inchi nzima sehemu palipokuwa na uchaguzi na sehemu nyingi
palikuwa hapana uchaguzi wowote. Lengo la operationi hiyo lilikuwa ni
kutoa elimu ya uraia ambayo raia wengi wanaikosa na kwamba elimu kama
hii huwa haitolewi na chama tawala kwa makusudi kudhihirisha ule usemi
wa Kiswahili unaosema USIMWAMUSHE ALIYELALA UKIMWAMSHA UTALALA WEWE.
Kikubwa
katika zoezi hilo ilikuwa kutoa elimu ya uraia kuhusu mchakato mzima wa
kuandika katiba mpya na ni nini wajibu wa raia kuhusu zoezi hilo
kikubwa kilichoongelewa ni:
a. Hali zoofu ya muungano baada ya
Zanzibar kuandika katiba yao ambayo imepelekea muungano kudhoofu sana
umekuwa muungano jina tu.
b. Chama tawala CCM kuteka nyara
mamlaka ya tume maalumu ya rais iliyokuwa inakusanya maoni toka kwa raia
ilimaarufu tume ya Jaji Warioba, operationi hiyo ya CHADEMA ilikuwa
inawafungua macho wanainchi waone jinsi chama tawala kinavyojitahidi
kuingilia mchakato huo kwa manufaa ya wachache badala ya manufaa ya
taifa zima na vizazi vyake.
c. Sehemu kulikokuwa na uchaguzi
wa madiwami CHADEMA ilifanya kampeni pamoja na kutoa elimu hii ya uraia,
nafikiri wanainchi wanajionea wenyewe sasa uhuni unaoendelea kenye
bunge maalumu la katiba unaoasisiwa na chama tawala mwenye macho
haimbiwi tazama.
Matokeo ya uchaguzi wa katika kata 27 uofanyika tarehe 8 February
Chama
cha CHADEMA kiliibuka na ushindi mnono kuliko Lumumba wanavyofiria hadi
kuitisha kikao na waandishi wa habari eti kuwashukuru wanainchi kwa
kuendelea kuwaamini mkutano ulioitishwa na domo kaya wao Nape Nnawiye.
Siyo kweli eti CCM Ilishinda uchaguzi huo ukweli ni kwamba CCM
ilishindwa vibaya kwa sababu za kisayansi zifuatazo;
a.
Katika sehemu CCM ilikoshinda kata za vijijini wanainchi wake
hawajitambui, hawajui kinachoendelea pembeni yao, hawana habari ,
wanafichwa , hawaelimishwi, hawajui hata matukio, mfano tuliwauliza ni
wapi mwenyekiti wa CCM alipigwa na mawe na wanainchi wenye hasira ,
alipigwa kama mwizi hadi akafa? Hawajui. Pia tuliwauliza ni mbunge gani
wa CCM anatuhumiwa kubaka na kumwambukiza mtoto wa shule UKIMWI?
Hawajui. Sasa ukishinda uchaguzi maeneo ya watu kama hao na wewe
utajihesabu umeshinda?
b. Katika sehemu CHADEMA ilikoshinda
zile kata tatu yaani Sombetini Arusha , Kiborloni Moshi na Njombe mjini
kata hizi wanaichi wake wanajitambua kata hizi thamani yake ni Dhahabu
na ninafikiri wana bodi mnafahamu kwamba katika mashindano ya Olympic
inchi moja ikishinda medali za dhahabu 3 na ingini ishinde medali za
fedha 200 kama CCM ilivyofanya basi ile iliyoshinda dhahabu inakuwa juu
sasa leo iweje CCM itake kudai ushindi katika uchaguzi huo wakati
iliambulia medali za fedha tu ? Shame on them.
Hitimisho
Chama
cha CHADEMA kinajivunia na kitaendelea kujivunia mafanikio kiliyopata
katika zoezi la M4C-OUD kwani kimesambaza elimu ya uraia , wanainchi
wanaendelea kufunguka macho na sasa wanajionea wenyewe uhuni
unaofanyiaka katika bunge maalumu la katiba na ni wazi kwa wale wote
wanaojitambua wanajua uhuni huo sababu yake ni nini. Pili kilipata
ushindi mnono na kunyakua medali zote 3 za dhahabu katika uchaguzi wa
madiwani uliopita, CCM iliambulia fedha na shaba tu, hebu waje hapa
akina Nape na Ngulu Mchemba wakanushe hili.
Aksanteni
Toka kurugenzi ya habari ya CHADEMA
Leo hii 7/3/2014.
No comments:
Post a Comment