Dar es Salaam. Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) imewahisha kwa siku 10, mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ili kupitisha maandalizi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Katika mabadiliko hayo mechi ya Simba dhidi yaCoastal Union ya Tanga iliyokuwa ichezwe leo kwenye Uwanja wa Taifa sasa itafanyika Machi 23.
Jana TPLB lilifanya marekebisho kwa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), ambapo sasa ligi hiyo itamalizika Aprili 19 badala ya Aprili 27.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo mpya mechi ya Simba na Yanga itakuwa imewahi kuwa siku 10, sambamba na mechi nyingine za kumaliza ligi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Boniface Wambura alisema marekebisho hayo yamefanyika, ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kujiandaa kwa mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika 2015, huku Stars ikitarajiwa kuanzia raundi ya awali Mei mwaka huu.
“Bodi imefanya marekebisho hayo kwa kuzingatia majukumu ya Taifa Stars, ambapo itaanzia hatua ya awali, kutokana na kuwa katika nafasi 30 boraAfrika. Tutaanza maandalizi mapema ya kuiandaa timu,” alisema Wambura.
“Jumamosi hii kutakuwa na mechi mbili baina ya Azam na Coastal Union, itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex, huku Yanga ikivaana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Baadhi ya marekebisho mengine ni Yanga kuvaana na Azam FC Machi 19, huku Yanga ikipambana na Tanzania Prisons Machi 26. Mechi zote zitafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Pia, Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 kwenye uwanja wa Mkwakwani, na Aprili 9 na Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22, kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi).
Machi 23, ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi 29 itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5, kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex).
Aprili 6, ni Coastal vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Raundi 25 itaanza Aprili 12, kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine).
Wakati Aprili 13 ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Pazia la ligi hiyo litafungwa Aprili 19, kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment