Joseph Haule a.k.a Profesa J au Wamitulinga akichana mistari wakati wa sherehe za Shirika la Daraja zilizofanyika kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe Jumamosi Machi Mosi, 2014. Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Njombe linajihusisha na shughuli za kijamii katika kuhimiza Utawala Bora, Uwazi na namna ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, hasa wa vijijini. Pia linachapisha gazeti la Daraja Letu ambalo ni maalum kwa habari za vijijini likitoa pia fursa kwa wananchi kutoa maoni yao.
Profesa J akiendelea kuchana.
Wasanii mbalimbali wa ngoma walipamba jukwaa siku hiyo.
"Imependeza eeeeh?" Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa picha hii wakati Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Daraja, Josephine Lemoyan (kushoto) akimuuliza Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Simon Mkina 'Mzee wa Tajoa' wakati wa sherehe hizo zilizofana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Daraja, Simon Mkina, akinena na wananchi wa Njombe kuhusu mafanikio ya shirika hilo wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini humo Machi Mosi, 2014. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kapteni (mstaafu) Assery Msangi na kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Josephine Lemoyan.
Mgeni rasmi katika sherehe za Daraja Day, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni (mstaafu) Assery Msangi, akifungua rasmi sherehe hizo.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Rachel a.k.a Kiuno Bila Mfupa Namba 2, naye alikuwepo kuhanikiza burudani. Ilikuwa balaa mwanangu.
He! Mkina amekuwa msanii tena? Hapana, hapa Mkurugenzi wa Daraja, Simon Mkina akinena na wakazi wa Njombe wakati burudani ikiendelea.
Mashabiki wakiserebuka uwanjani.
Kundi la ngoma za asili ambalo nalo lilipamba sherehe hizo.
Wananchama wa Klabu ya Twanga Swali nao walifanya mambo yao.
Wasanii wa vicheko wakionyesha mbwembwe zao huku wakisoma gazeti la Daraja Letu.
No comments:
Post a Comment