Olivier Giroud na Mesut Ozil wakishangilia bao la nne kwa Arsenal dhidi ya Everton katika dakika ya 85. Bao hilo limefungwa na Giroud.
Olivier Giroud akishangilia bao la tatu kwa Arsenal alilofunga dakika ya 83.
Mikel Arteta akishangilia bao la pili kwa Arsenal alilolifunga kwa penalti katika dakika ya 67.
Romelu Lukaku wa Everton baada ya kuifungia timu yake bao dakika ya 32.
Santi Cazorla na Mesut Ozil wakifurahia bao la kwanza lililofungwa dakika ya 7 na Ozil.
TIMU ya Arsenal imeibuka kifua mbele kwa bao 4-1 dhidi ya Everton kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la FA iliyopigwa Emirates hivi punde! Kwa matokeo hayo, Arsenal wametinga Nusu Fainali ya michuano hiyo.
GPL
No comments:
Post a Comment