
Uwanja wa Wembley
Uwanja wa Wembley ulioko Uingereza utakuwa mwenyeji wa nusu fainali ya Kombe la Euro2020, Uefa imethibitisha.
Wembley pamoja na uwanja ulioko Glasgow, Hampden Park
na ule ulioko Dublin, Aviva zitaandaa mechi 16 na tatu zingine za makundi.
Shirikisho la Soka la Uingereza lilipewa uenyeji wa mechi hiyo baada ya kuishinda shirikisho la Ujerumani.
Hata hivyo Shirikisho hilo litapata fursa ya kuandaa mechi kadha za makundi.
Haya yalibainika baada ya Uefa kutangaza viwanja 13 vitakavyoandaa mechi za Euro .
Mechi za robo fainali na tatu za makundi zitaandaliwa mjini Munich (Ujerumani), Baku (Azerbaijan), Roma (Italia) na St Petersburg (Urusi).
Miji mingine itakayoandaa mechi 3 za makundi na moja ya mkondo wa pili ni Copenhagen (Denmark), Bucharest (Romania), Amsterdam (Uholanzi), Bilbao (Uhispania), Budapest (Hungary) na Brussels (Ubeljiji).
CREDIT: BBC/MICHEZO
No comments:
Post a Comment