Mkurugenzi wa Prime Time na meneja wa vipindi wa Radio Clouds FM Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa mwanamuziki wa Marekani TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika Dar es Salaam mwezi ujao.
Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Allan Chonjo akizungunza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakimtangaza mwanamuziki TI atakayeshiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Mkurugenzi Mkuu wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Efraim Mafuru (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Ruge Mutahaba katika hoteli ya Serena wakati wa kumtambulisha msanii TI wa Marekani ambaye atashiriki tamasha la Fiesta litakalofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
Mwanamuziki
wa Kimarekani katika miondoka ya Hip-hop ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki,
mwigizaji na mwekezaji, Clifford Joseph Harris Jr, alimaarufu kama T.I.
amethibitishwa rasmi na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd (SBL)kama mwanamuziki
wa kimataifa atakayetumbuiza katika kilele cha shangwe za Serengeti Fiesta
zitakazofanyika jijini Dar es salaam tarehe 18 Oktoba mwaka huu.
Katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya SBL, Meneja Masoko
Allan Chonjo alisema, " hivi karibuni tumetia saini na kukamilisha mikataba
yote ili kuhakikisha kwamba mwanamuziki huyu wa kimarekani anafika Leaders Club
jijini Dar essalaam tarehe husika"
Chonjo
aliendelea kusema, 'Tungependa kuwashukuru washirika wetu, Prime Time
Promotions kwa kuhakikisha tunakamilisha mikataba yote na vile vile kwa
kuhakikisha kamba tamaha hili linakamilika kwa mafanikio. Hii itakuwa ni mara
ya kwanza kwamba T.I kutia mguu wake katika ardhi ya Tanzania.
Akizungumza
na vyombo vya habari, Sebastian Maganga kutoka Prime Time Promotions, alikuwa
na haya ya kusema, "kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa tukihakikisha kwamba
tunaelewa nini watanzania wanataka na tumekuwa tukijitahidi bila kuchoka
kuhakikisha kamba tukio tunalolifanya, kwa mwaka huu, wapenzi wetu watashuhudia
shoo ya nguvu ambayo haijawahi yanyika hapa nchini.
"Mpaka
sasa, Serengeti imetembelea mikoa kumi (10) nchini, na itaendelea na ziara hiyo
katika mikoa ya Singida, Songea, Mtwara, Dodoma na Mbeya.
Katika
mabadiliko mengine Serengeti Breweries na Prime Time Promotions wamewaomba
mashabikiwachague msanii wa kitanzania ambaye wangependa atumbuize na TI. “Hiki
ni kitu kipya natunataka kuhakikisha kwamba mashabiki wanaburudika vya kutosha,
alisema Maganga. ‘Habari zitasambazwa kwa njia ya TV na redio kuelezea jinsi ya
kushiriki’, aliongeza.
Serengeti Fiesta inatambulika kwa kuleta wasanii wa kimataifa hapa nchini,
miongoni mwao ni pamoja na Rick Ross, Shaggy na Davido
T.I
aliyetamba na kibao "No Mediocre" amekuwa akijishughulisha na shughuli
mbalimbali ikiwemo biashara. Yeye ni muasisi na mkurugenzi mkuu wa Grand Hustle
Records.
T.I. alianza
kupata umaarufu mwaka 2003, baada ya kushirikishwa na mwanamuziki mwenzake Bone Crusher, ambaye ni
mkazi wa Atlanta, katika wimbo wa "Never Scared". Alipata umaarufu
zaidi baada ya kutoa wimbo wa Trap Muzik (2003).
Mwaka 2004,
T.I. alionekana kwenye wimbo wa Destiny's Child's "Soldier", sambamba
na Lil Wayne. Albamu ya sita ya TI, Paper Trail (2008), ilikuwa albamu yake ya
mafanikio zaidi , na imefanikiwa kuuza nakala 568,000 katika wiki ya kwanza
nchini Marekani na kuifanya ya tatu katika chati ya albam bora nchini humo.
Mpaka sasa, T.I. amdeshinda tuzo tatu za Grammy Awards.
T.I. pia
ametoa nyimbo kama vile"Bring Em Out", "What You Know",
"Swagga Like Us" (akimshirikisha Kanye West, Jay-Z and Lil Wayne),
"Dead and Gone" (akimshirikisha Justin Timberlake), "Ball"
(akimshirikisha Lil Wayne) and "No Mediocre" (akimshirikisha Iggy
Azalea).
No comments:
Post a Comment