Barnaba Classic ndani ya Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
Godzilla ndani ya Uwanja wa Maji Maji akifanya vitu vyake
Maelfu
ya mashabiki wa mji wa Songea ijumaa iliyopita walikusanyika katika uwanja wa
Majimaji mjini humo kushuhudia shoo kali ya kihistoria iliyoporomoshwa na
wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
Kwa
mara ya kwanza katika historia, shoo ya Serengeti Fiesta iliingia katika viunga
vya mji wa songea na shoo kali zilizokonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa mji
huo mara baada ya kufanya shoo nyingine kali kwa mafanikio katika mji wa
morogoro.
Kama
ilivyo utamaduni wake wadhamini wakuu wa shoo hiyo kampuni ya bia ya Serengeti
kwa kutumia kinywaji chake kikuu Serengeti Premium Lager iliwapelekea mashabiki
wa mji huo wasanii nyota wanaotamba kwa sasa katika tasnia ya muziki wa kizazi
kipya, wengi wao wakitumbuiza katika mji huo kwa mara ya kwanza.
Godzilla,
TID, Linex, Mr. Blue, Madee, Stamina, Barnaba, Ney wa Mitego, Linah, Recho, Mo
Music na Baraka Da Prince ni baadhi ya wasanii waliokuwa wakisubiriwa kwa hamu
na wakazi Songea.
Mr Blue akiwapagawisha mashabiki ndani ya Uwanja wa Maji Maji, Songea
Mbali
na shoo hiyo, shughuli nyingine iliyofanyika ni Serengeti Super Nyota diva na
mshindi atapata nafasi ya kuja kushuhudia shoo ya mwisho itakayofanyika jijini
Dar es salaam mwezi ujao. Ilishangaza kuona vipaji vya ajabu walivyonavyo
vijana hao wa Songea.
Kadri
jioni ilivyokuwa ikikaribia ndivyo maelfu ya mashabiki walivyoendelea
kumiminika kwa kwa wingi kuja kushuhudia shoo hiyo, sehemu kubwa ya tiketi kwa
ajili ya kuingia kwenye tamasha hilo ziliendelea kununuliwa mapema kwenye
milango ya saa9 jioni kabla ya shoo kuanza.
Idadi
ya watu waliokuja kushuhudia tamasha la burudani la Serengeti Fiesta ilikuwa kubwa kiasi ambacho
kiliwashangaza hadi waandaji wa tamasha hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza
katika hitoria yake mkoani hapo.
Ney wa Mitego akiwa kazini
TID akishambulia jukwaa kwenye Uwanja wa Maji Maji
Uanzishwaji
wa screen za LED kubwa badala ya zile za kawaida zilizokuwa zikitumika hapo
awali zilionekana kuvuta hisia za wakazi wa mji wa Songea ambao wengi wao waliipongeza
Primetime Promotions kwa kufanya maandalizi mazuri.
Shoo
ilidumu kwa zaidi ya masaa nane. Godzilla, TID na Madee ni baadhi ya wasanii waliokonga
vilivyo nyoyo za mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo kabla ya msanii Ney wa
Mitego na Stamina kupanda jukwaani na wimbo wao walioshirikiana kuimba uitwao
“Huko kwenu vipi”.
“Napenda
kuwashukuru mashabiki wa mjini songea
kwa kujitokeza kwa wingi katika shoo hii….kiukweli ilinishangaza na nafurahi
kuwa hawakutuangusha ukichukulia kigezo kwamba shoo hiyo ilikuwa ikifanyika kwa
mara ya kwanza mjini hapa katika mtiririko wa shoo zake za mwaka huu za Serengeti
Fiesta”…alisema Rugambo Rodney – Meneja Chapa wa kinywaji cha Serengeti Premium
Lager.
Kwa
mwaka huu waandaaji wa tamasha hilo walichagua mikoa 18 ambayo shoo hiyo itapita
na hii ni idadi kubwa ya mikoa iliyochaguliwa katika historia ya tamasha hilo,
mikoa iliyoongozeka ni 3 katika ratiba za tamasha hilo, nayo ni Bukoba, Kahama
na Songea.
Baada
ya Songea, tamasha la Serengeti Fiesta 2014 litaelekea na shoo zake katika mikoa
ya Mtwara, Mbeya, Dodoma, Singida likiwa na kauli mbiu yake “sambaza upendo” kabla
ya kuhitimishwa rasmi jijini Dar tarehe
18 Oktoba ambapo wasanii wa nyumbani
watapata nafasi ya kutumbuiza jukwaa moja na msanii toka Marekani T.I ambaye
kwasasa anaetamba na kibao chake “No mediocre”.
No comments:
Post a Comment