Katibu wa NEC (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye
NA MARY GEOFREY
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Mfumo wa Uandikishaji na Uhakiki wa Wapiga kura (BVR) ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) inataka kuutumia kwenye kuandikisha upya majina ya wapiga kura ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kadhalika, kimesema ni mfumo ambao umeundwa na watu wachache ili kujitengenezea ulaji na siyo kurahisisha zoezi la upigaji kura na njia mbadala ni kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (Nida) ili kupunguza gharama za uandikishaji.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Chalinze, mkoani Pwani jana, Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema mfumo huo wa Biometric hautarahisisha uchaguzi kama ilivyoelezwa na tume, bali unaongeza gharama na siyo wa uhakika kwa uchaguzi.
“Mfumo huu umeshaleta matatizo katika chaguzi za nchi mbalimbali zilizowahi kuutumia ikiwamo, Kenya, Ghana na Malawi, hivyo hauwezi kusaidia kwenye uchaguzi, kinachoonekana hapa kuna ulaji na watu wachache ndio watakaofadika nao na kuongeza gharama zisizokuwa na msingi,” alisema.
Nape alisema mfumo wa BVR lazima utaleta matatizo kwenye uchaguzi mkuu ujao na itaonekana ni njama ambayo CCM wameipanga ili washinde katika chaguzi hizo hivyo ni bora kuukataa sasa kabla haujaanza kufanya kazi kwa kuwa wameshajua ni mbovu na kwamba CCM inataka kushinda kwa haki.
“Huu mfumo siyo mzuri hasa kwa nchi kama yetu ambayo hakuna umeme wa uhakika, tuache kuiga mambo ambayo nchini nyingine zilishindwa na hata sisi hatuyawezi,” alisema Nape.
Alisema ni vyema nchi ikajifunza kwa nchi nyingine walioutumia mfumo huo, ambako kote haukufanikiwa ikizingatiwa kuwa nchi hizo zina teknolojia nyingi.
Nape alisema, ni vyema Nida na tume kukaa meza moja, ili kuangalia namna ya kutumia vitambulisho vya taifa kuliko kuandaa mfumo wa kutengeneza vingine ambavyo alama zitakazochukuliwa ni kama wanazochukua watu wa Nida.
“Ukiachilia mbali gharama za kutengeneza vitambulisho hivi, nchi sasa iko kwenye mfumo wa teknolojia, kitambulisho kimoja kinatumika kufanyia shughuli zote, lakini hapa nchini tunaendeleza mfumo wa zamani, mwisho wa siku tutajikuta tunatembea na lundo la vitambulisho kwenye pochi,” alisema Nape.
Alisema tume ilishakaa vikao vinne ili kuangalia namna na kuachana na mfumo huu lakini muafaka haujapatika na muda umekwisha.
“Inavyoonekana hapa kuna ulaji ndiyo maana hawa watu hawataki kukaa kuzungumza na wanapaswa kutambua kuwa serikali haina fedha kama wana dili zao haziwezi kufanikiwa, mwisho wa siku watasema CCM tumetengeneza mazingira ya kuiba kura,” alisema.
Nape alifafanua kuwa nia ya dhati ya CCM ni kuwa haki itendeke na kila chama kishinde kwa haki.
Alisema mfumo huo, ulishaanza kutia dosari baada ya tume kuutangaza na ukaonekana na wapinzani ni njia ya CCM kuiba kura jambo ambalo halikuwa kweli.
Pia, alisema licha ya tume kuomba Sh. bilioni 200 za kuendesha zoezi hilo, lakini hadi sasa imetengewa Sh. bilioni 7 fedha ambazo hazijafika hata robo ya mahitaji yote, hivyo ni vyema wakatumia kitambulisho kimoja kuliko kuiingizia hasara serikali.
“Tukiangalia zoezi la Nida linavyokwenda linawapotezea watu muda, leo tena uje uwashindishe watu kwenye vituo vya kuandikisha vitambulisho vya kura, wananchi watafanya maendeleo saa ngapi?” alihoji Nape.
Aidha, aliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, ihakikishe inawakutanisha Nida na tume ili kutumia takwimu zilizopo.
“Suala hili liko chini ya Waziri Mkuu, ni vyema akakaa nao meza moja na muafaka ukapatikana,” alisema Nape yupo kwenye ziara mkoani hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kufuatilia utekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2010/15.
MALALAMIKO YA VYAMA VINGINE
Aprili, mwaka huu, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Freeman Mbowe, akiwasilisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kuna mchakato wa maandalizi ya siri unaoendeshwa na Nec wa kuandaa utambulizi wa wapiga kura kwa kutumia mfumo wa Biometric wa kumtambua mpiga kura kwa alama za mwili kama vidole au mboni ua jicho.
Hivi karibuni, wakati wa Mkutano Mkuu wa Chadema, alisema hakuna ushirikishwaji wa vyama vya upinzania katika mchakato wa mfumo mpya huku akidai CCM kikishirikishwa kikamilifu.
KAULI YA NEC
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alisema mfumo wa awali wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura ulilalamikiwa na vyama vya upinzania na kuona haufanyi kazi kwa haki ndiyo maana wakakutana na wadau wote vikiwamo vyama vyote vya siasa na kuwaeleza juu ya mfumo wa BVR ambao utakuwa wa kielektroniki.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment