Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 30 September 2014

BAADA YA 'MCHINA' KUWADHURU, WANAWAKE WA TANZANIA SASA WAFURIKA AFRIKA KUSINI KUTENGENEZA MAKALIO NA MATITI


WANAWAKE wa Tanzania ni miongoni mwa wanawake wengi barani Afrika wanaofurika nchini Afrika Kusini kwa madaktari wa kienyeji kutengeneza matiti ili yafanane na ya Kim Kardashian, makalio kama ya Jennifer Lopez na tumbo kama la Jessica Alba.
Safari za Operesheni hizo nchini Afrika Kusini kwa sasa siyo za matajiri kama ilivyokuwa zamani kwa Wamarekani na Wazungu kutoka Ulaya, na akinadada hao wanatumia mpaka Randi 100,000 (takriban Shs. 25 milioni za Tanzania) kwa ajili ya upasuaji huo.

Operesheni ya kuongeza makalio 
Takriban miaka 10 iliyopita wanawake wengi wa Tanzania walikuwa wamezama kwenye matumizi ya dawa za Kichina kuongeza makali na matiti, lakini wengi kati ya watumiaji hao walipata madhara makubwa ya matiti kutepeta, makalio kupishana na mambo mengine kama hayo.
Athari za makalio yaliyotokana na dawa za Kichina

Mawakala wanaohusika na safari za operesheni za aina hiyo wamesema kumekuweko na ongezeko kubwa la wanawake hasa kutoka Tanzania, Zambia, Ghana, Kenya, Nigeria na Angola wakitaka kuongezewa matiti, makalio, kupunguza tumbo na hata kutengeneza midomo.
Pia wanawake hao wanatumia safari hizo kwa ajili ya kununua nguo za kisasa, viatu, mikoba, almasi na kadhalika, ikiwa ni njia ya kuwazuga watu wengine kwamba hawakwenda huko kwa ajili ya upasuaji huo.
Daktari bingwa wa upasuaji huo kutoka Sandton, Dk. Chetan Patel anasema operesheni za kupunguza na kukuza matiti zilikuwa maarufu kwa wanawake kutoka Msumbiji. Urekebishaji wa midomo pamoja na kuongeza makalio pia kulikuwa na idadi kubwa ya wahitaji.
"Umbile la mwili katika tamaduni za Kiafrika linachukuliwa kwa umuhimu mkubwa sana katika suala la urembo kuliko urembo wa bandia," anasema Patel.
"Waafrika kwa ujumla wana ngozi nzuri kuliko watu weupe na kwa hiyo operesheni za kutengeneza sura na maumbile huwa hazipewi umuhimu mkubwa."
Anasema amekuwa na maombi mengi sana ya wanawake wanaotaka kuwa na makalio kama yale ya Lopez na Kardashian. "Unatakiwa kutathmini maombi na matarajio ya mgonjwa na kulinganisha na maumbile ya miili yao kama hilo linawezekana."
Patel anasema utengenezaji wa maumbile bandia kwa sasa siyo utamaduni wa Kimagharibi pekee. "Kwa kadiri Waafrika wengi walivyoathiriwa na vyombo vya habari na ule utamaduni wa nyota wa Hollywood, kwa hiyo matamanio yao ya kulingana na nyota hao yameongezeka.
"Wakichagizwa na ongezeko la kipato... Waafrika wanatafuta namna ya kufikia kwenye mambo makubwa ambayo hawakuwa wakiyafikiria kabla."
Dk. Paul Skoll wa Cape Town anasema wateja wake kutoka Angola na Msumbiji wameongezeka sana, huku wengi wao wakitaka kuongezewa ama kupunguziwa matiti, midomo na makalio.
Amesema pia anapokea maombi kutoka kwa Wabrazili ili kuwa na maumbile kama ya Kardashian, Lopez au Nicki Minaj.
Skoll anasema anawatoza wateja wake kulingana na mahitaji ya kila mmoja wao.
Lorraine Melvill, mkuu wa kampuni ya Surgeon and Safari, wakala anayehusika na kuandaa mazingira ya watu kufika Afrika Kusini kwa ajili ya upasuaji, alisema wengi kati ya wateja wake wanatoka Zambia na wengi wao walitaka kuongezewa makalio.
"Tunapokea maombi mengi, lakini wakati mwingine hayana uhakika. Mtaalam anashughulikia utaalamu alionao na kila mteja ana mahitaji yake tofauti."
Denise Milner wa kituo cha Surgical Bliss, kilichopo Cape Town, anasema wateja wake wakubwa wanatoka Angola, Tanzania, Kenya na Nigeria.
"Waafrika hawataki na hawana mpango wa kutengeza nyuso zao. Daima wanataka kutengeneza matiti na makalio," alisema Milner, ambaye pia hushughulikia matatizo ya uzazi.
Alisema wateja wake wa Kiafrika wanatumia kati ya Randi 40,000 na 100,000 kwa operesheni hizo - wakati mwingine mara mbili kwa safari moja - na malazi.
CREDIT: http://www.timeslive.co.za/lifestyle/2014/09/22/africans-flocking-to-south-africa-for-bigger-boobs-butts-surgery

No comments:

Post a Comment