Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 23 September 2014

NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI ARUSHA LEO

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini, Pereira Ame Silima. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment