Mamia ya waandamanaj wa Hong Kong wamezingirwa na Askari polisi wanaowataka kusitisha maandamano na mkusanyiko wao karibu na ofisi za Makao makuu ya serikali.
Waratibu wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na kuwataka watu wengine zaidi kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai yao ya kuitaka China iwaachie uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017.
Kiongozi wa Mamlaka ya Hong Kong C Y Leung amesema serikali yake imesikiliza na kuzingatia madai ya waandamani lakini inapingana na mpango wao wa kujitenga.
‘’Mimi na serikali yangu tutazingatia sheria za msingi na uamuzi unaostahili wa NPCSC,tutajaribu juhudi zote kutekeleza uchaguzi wa kiongozi mkuu kwa kila anayestahili kupiga kura atafanya hivyo mwaka 2017. Serikali itaanzisha hatua inayofuata ya majadiliano kuboresha katiba hivi hivi karibuni. Inasihi sekta mbalimbali za jamii kushiriki katika majadiliano yenye mantiki kwa Amani na kwa kufuata sheria, kufikia makubaliano na kukubali tofauti pamoja na kuruhusu watu milion tano wenye uhalali wa kupiga kura hapa Hong Kong kumchagua kiongozi mkuu mwaka 2017 mtu mmoja kura moja’' amesema Leung Chung-ying.
‘mimi na serikali yangu tumekuwa wasikivu kwa raia na tumejitolea kudumisha jamii yote. Wananchi wanatakiwa kutoa wanayoyahitaji kwa Amani, mantiki na kisheria, na kuheshimu na kuzingatia mitazamo mbalimbali katika jamii. Serikali ya SAR ya Hongkong imeazimia kupinga utawala usio wa kisheria wa ofisi za serikali kuu au makao makuu ya wilaya ‘utawala wa seriakli kuu’’. Polisi wanajitambua kukabiliana na hali kwa wakati kwakuzingatia sheria’’ Ameongeza
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment