Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 28 September 2014

JIVU LA VOLCANO LAWAUA WATU 30 JAPAN


Mlima Ontake

Takriban wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo.
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha Mlima Ontake.


Wakwea milima katika Mlima Ontake

Waokoaji hao wamefanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo ambapo ndege ya kijeshi aina ya helikopta ilitumiwa kuwaokoa karibu watu 40 waliokuwa wamejeruhiwa.
Zaidi ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwenye mlima huo wenye urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila ya kutoa onyo lolote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment