Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tawi la Kimara Korogwe jijini Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya kupinga vikao vya Bunge la Katiba vinavyo endelea mjini Dodoma.
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tawi la Kimara Korogwe jijini Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya kupinga vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Korogwe jana kimefanikiwa kufanya maandamano yaliyoanzia eneo la Korogwe hadi Kimara Baruti kupinga Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Hata hivyo maandamano hayo yaliyodumu kwa dakika 45 yalisambaratika yalipo fika Kimara Baruti baada ya polisi walikuwa katika gari lao kufika eneo hilo.
Maandamano hayo yalianzia Korogwe saa 3 na dakika 45 asubuhi yalipangwa kuishia ofisi ya chama hicho ya Kimara Baruti ambapo wafuasi zaidi ya 50 wa chama hicho wakiwa na mabango yenye ujumbe tofautitofauti walijumuika.
Hata hivyo inadaiwa viongozi wa chama hicho wa kata hiyo walioratibu maandamano hayo walitoweka muda mfupi baada ya kuanza kwa maandamano hayo kukwepa wasikamatwe.
Mmoja wa wanachama wa chama hicho ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kwamba lengo la ilikuwa ni kuandamana kufikisha ujumbe kwa wananchi wa kupinga bunge hilo.
"Tutaendelea kufanya maandamano hata kwa dakika 10 ili mradi tufikishe ujumbe wetu kwa njia ya amani na kesho 'leo' tutafanya Kata ya Manzese na kata nyingine" alisema mwanachama hao.
Alisema wataendelea kutumia mbinu hiyo ya kushitukiza kufanya maandamano hayo kama walivyofanikiwa katika kata hiyo ya Korogwe mpaka kieleweke.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillius Wambura amethibitisha wanachama hao kufanya maandamano hayo.
"Ni kweli wafuasi hao wa chadema wamefanya maandamano hayo katika eneo hilo lakini hakuna mwanachama aliyekamatwa" alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment