Ofisa wa Jeshi la Polisi kutoka Kitengo cha kuzuia Madawa ya Kulevya mkoani Arusha D/CPL Kaleb akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) magunia yaliyokuwa na dawa za kulevya aina ya bangi iliyokuwa inasafirishwa kutoka Arusha kwenda mkoani Tanga.
MNAMO TAREHE23/09/2014 MUDA WA SAA 23:00 USIKU KATIKA MAENEO YA NDURUMA HALMASHAURI YA JIJILA ARUSHA, JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUPITIA KITENGO CHA KUZUIA MADAWA YAKULEVYA TULIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WAWILI AMBAO NI LAIZER S/O MELAU (35) MKAZI WA ORKOKORA NA RICHARD S/O FANUEL (38) DEREVA NA MKAZI WA MIANZINI WAKIWA WANASAFIRISHAMADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA MANNE YENYE JUMLA YA UZITO WA KILOGRAMU173 KWA KUTUMIA GARI AINA YA TOYOTACOROLLA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.592 AAP.
MAFANIKIO HAYO YALIPATAKANABAADA YA WANANCHI AMBAO NI RAIA WEMA KUENDELEA KUWA KARIBU NA JESHI LA POLISIAMBAPO WALITOA TAARIFA JUU YA TUKIO HILO NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUANZAKULIFANYIA KAZI KWA KUWEKA MTEGO MAENEO YA NDURUMA.
MARA BAADA YAKULIONA GARI HILO WALILISIMAMISHA NA WALIPOFANYA UPEKUZI WALIYAONA MAGUNIA HAYOMANNE NDANI YA GARI HILO, KATI YA HAYO MATATU YALIKUWA KWENYE ‘’SEAT’’ YAKATIKATI NA MOJA LILIKUWA KWENYE ‘’BOOT’’. KATIKA MAHOJIANO WATUHUMIWAHAO WALIKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO NA WALISEMA KWAMBA, WALIKUWA WANAYAPELEKAMKOANI TANGA. UPELELEZI WA TUKIO.
HILI BADO UNAENDELEA NA MARA UTAKAPOKAMILIKAWATUHUMIWA HAO WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AHSANTENIKWA KUNISIKILIZA. IMETOLEWANA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHAKAMISHNAMSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI(SACP)LIBERATUS SABASTAREHE25/09/2014.
No comments:
Post a Comment