Barnaba Classic kuhanikiza katika Uwanja wa Sokoine leo
Kusubiri sasa kumetosha kwa wakazi wa Mbeya na
vitongoji vyake, kinywaji cha Serengeti Premium Lager kwa kushirikiana na
waandaji wa tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Primetime Promotions wameshaingia
mjini humo kuporomosha burudani ya aina yake katika uwanja wa Sokoine leo.
Baada ya kugundua kwamba tamasha la Serengeti
Fiesta litakuwa mkoani humo mwishoni mwa juma hili, wakazi wa mji wa Mbeya wamejipanga
tayari kwa ajili ya kulipokea tamasha hilo na mashabiki wengi wameahidi
kufurika katika uwanja huo.
Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 linatarajia kuweka
historia kwa kuvuta idadi kubwa ya mashabiki toka sehemu mbalimbali za mkoa huo.
Kwa Mbeya tamasha hilo litatimiza shoo ya 14 kati ya 18 walizoahidi waandaaji.
Shoo hiyo inayosubiriwa kwa hamu mjini Mbeya itapomorohwa
na wasanii wakali katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya kama “Godzilla,
TID, Linex, Mr. Blue, Madee, Stamina, Barnaba, Ney wa Mitego, Linah, Recho, Mo
Music na Baraka Da Prince ambao wameahidi kufanya shoo ya aina ya kipekee.
“Katika kumbukumbu zetu, Mbeya ni mkoa ambao siku
zote huandika historia mpya kwa kuingiza idadi kubwa ya mashabiki katika shoo za
tamasha la Serengeti Fiesta. Ni matarajio yangu kuwa kwa mwaka huu pia
mashabiki wetu wa mbeya watavunja tena historia ya miaka iliyopita kwa kuja kwa
wingi,” alisema Rugambo Rodney, Meneja Chapa wa kinywaji cha Serengeti Premium
Lager.
Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wasanii
ambaye anatarajiwa kutuimbuiza mjini hapa Mbeya, Godzilla alisema… “Awali ya
yote, ninashukuru kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza tamasha la Serengeti
Fiesta mwaka huu na zaidi ya yote, kitendo cha kutumbuiza nyumbani hakika
kimenipa faraja sana. Napenda kuwahakikishia mashabiki wangu kuwa shoo yangu hapa
Mbeya itakuwa moja ya shoo bora na kwamba kijana wenu wa nyumbani
hatawaangusha, hivyo tukutane uwanja wa Sokoine na tuburudike kwa pamoja.”
Baada ya Mbeya, Serengeti Fiesta itaelekea Dodoma
na Singida na kuhitimisha ziara yake jijini dar es Salaam hapo Oktoba 18.
No comments:
Post a Comment