Na Julius Konala wa demasho.com, Songea
WAKAZI wa Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma, wataondokana na tatizo la upatikanaji wa maji lililowakumba kwa muda mrefu hususan kipindi cha kiangazi baada ya kuanza
kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kitega maji.
Mradi huo ulioko katika eneo la Ruhira mjini humo unaotekelezwa na kampuni ya Sinani Building Contactors Ltd yenye makao yake makuu mkoani Mtwara utagharimu kiasi cha zaidi ya Shs. 2 bilioni mpaka kukamilika kwake.
Mradi huo ulioko katika eneo la Ruhira mjini humo unaotekelezwa na kampuni ya Sinani Building Contactors Ltd yenye makao yake makuu mkoani Mtwara utagharimu kiasi cha zaidi ya Shs. 2 bilioni mpaka kukamilika kwake.
Hayo
yalisemwa jana na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Souwasa) Manispaa ya Songea, Mhandisi John Kapinga, wakati
alipokuwa akizungumza na baadhi
ya waandishi
wa habari ofisini kwake kuelezea utekelezaji wa
mradi huo.
Kapinga
alisema kuwa mradi huo mpaka
kukamilika kwake unatarajia kukidhi mahitaji ya wakazi wa Manispaa hiyo
kwa asilimia 60, kusukuma maji lita 6,500 pamoja na kuhifadhi lita zaidi
ya 800,000 za maji jambo ambalo amesema litasaidia kupunguza tatizo
la mgao wa maji kwa wakazi hao.
Alisema
kuwa tatizo kubwa linaloukabili mradi huo ni juu ya upatikanaji wa
fedha kwa ajili ya kumlipa Mhandisi Mshauri na Mkandarasi jambo ambalo
amedai lisipochukuliwa hatua za haraka linaweza kukwamisha maendeleo ya
ujenzi wa mradi huo ikizingatiwa bado kipindi kifupi cha kuanza msimu wa
kifuku.
Naye
Mhandisi wa kampuni ya Sinani Building Contactors Ltd inayojenga
mradi huo, Faustin Otaru alisema kuwa kati ya kazi zinazofanyika hivi
sasa ni kuchimba mitalo kwa ajili ya kujenga ukuta katika eneo hilo la
mradi lenye ukubwa wa mita za mraba 25,000.
Otaru
alizitaja changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wao wa kazi
kuwa ni pamoja na kutitia kwa mitambo ya kufanyia kazi,ubovu wa njia za
kuingilia magari kwenye eneo la mradi pamoja na ucheleweshwaji wa fedha
za kufanyia kazi jambo ambalo amedai kuwa linaweza kukwamisha maendeleo
ya mradi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Waandishi wa habari hao katika eneo la mradi
baadhi ya wakazi wanaozunguka eneo la mradi huo walisema kuwa kukamilika
kwa mradi huo kutasaidia kupunguza tatizo la maji na kudai
kwamba wameweza
kunufaika na
kampuni hiyo kwa kupata ajira ambayo imewawezesha kufanya mambo
mbalimbali ikwemo kusomesha na kulipa kodi katika nyumba walizopanga.
No comments:
Post a Comment