Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 24 September 2014

SERENGETI YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA 'JEBEL COCONUT'

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL), Ephraim Mafuru katikati akifafanua  jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Steven Gennon (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kinywaji kipya cha Jebel Coconut, ambacho ni pombe kali.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Steven Gannon akitoa uafafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya kinywaji kipya cha pombe kali aina ya Jebel Coconut, mara baada ya uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti(SBL), Ephraim Mafuru (kulia) akiwamiminia waandishi wa habari kinywaji kipya ambacho ni pombe kali aina ya Jebel Coconut mara baada uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) moja ya kampuni kubwa za kutengeneza bia nchini na watengenezaji wa bia maarufu aina ya Serengeti Premium Lager wametangaza rasmi kuzindua bidhaa yao mpya inayoitwa Jebel Coconut.
Jebel ni kinywaji kipya aina ya pombe kali kilichobuniwa Tanzania na kutengenezwa kwa ladha ya nazi, ambazo hupatikanan kwa kirahisi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Steve Gannon alisema, “Sisi tunayo furaha ya kuzindua bidhaa mpya katika soko baada ya kufanya tafiti nyingi juu ya mahitaji ya wanywaji nchini Tanzania na kubaini kuwa kuna pengo katika mahitaji yao.”
Jebel ilibuniwa hapa Dar es salaam kutokana na mandhari yake ya ufukweni na ndio maana ya kuja na kauli mbiu ya “Full Kipupwe”. Kinywaji hiki ni cha kwanza kubuniwa hapa nchini kati ya pombe kali zaidi ya 10 za kimataifa zinazosambazwa na kampuni hiyo. Walengwa haswa wa kinywaji hiki ni watu wazima wenye umri wa kati na SBL ina uhakuka kwamba soko litaipokea vizuri bidhaa hii kutokana na ladha, ubora na bei yake mradufu. Jebel ina ladha ya kipekee na inaweza kunyweka kwa ilivyo au ikachanganywa na barafu na kwa wengine soda ya tangawizi au ndimu.
Katika jitihada za kuhakikisha kuwa bidhaa inawafikia wanywaji walengwa hivi karibuni, Mkurugenzi wa Masoko, Ephrahim Mafuru alisema, "Hivi karibuni kutakuwa na shughuli nyingi ambazo zitampa nafasi mnywaji wa kitanzania kupata ladha ya ukweli na uhakika kwa hiyo wanywaji wanaalikwa kushiriki promosheni itayofanyika katika baa mbalimbali na maduka ili kuwapa nafasi wanywaji kujaribu ladha ya kipekee ya Jebel na kupata zawadi kemkem.”
Kinywaji hiki kipya cha Jebel kitaletwa katika chupa yenye ujazo wa 250ml na yenye rangi ya dhahabu, bluu na kijani kwa shilingi za kitanzania 3000 tu.

No comments:

Post a Comment