Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 7 September 2014

VIONGOZI WA DINI ZAIDI YA 1,000 KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI


Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha:
ZAIDI ya viongozi wa dini 1000 kutoka nchini mbalimbali barani Afrika wanatarajia kupewa elimu ya ujasiriamali lakini pia kukabidhiwa miradi kwenye nchi zao ili kuondokana na dhana ya kuwa viongozi wa dini hawana maendeleo kama walivyo watu wengine.
Pia mbali na kupewa elimu hiyo sanjari na kukabidhiwa kwa miradi viongozi hao watafunndishwa namna ya kuwafundisha waumini wao jinsi ya kubuni miradi mbalimbali.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa kongamano lililowahusisha viongozi wa dini kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika, Rais wa Umoja huo Miburo Celestin alisema kuwa zoezi hilo la kuwakomboa viongozi wa dini litaanza mapema mwakani
Alidai kuwa kupitia elimu na miradi mbalimbali ambayo watakabidhiwa viongozi wa dini ni lazima wananchi wataweza kupiga hatua kwa kiwango cha hali ya juu sana kwani kwa kupitia njia za taasisi za dini kama vile makanisa inakuwa ni raisi sana kuweza kuifikia jamii.
“Tunachotaka sisi ni kuwa mtu akiitwa kiongozi wa dini basi awe ni watofauti sio una muhubiria mtu kuwa anatakiwa kuachana na umaskini halafu yeye ni maskini wa kutupa sasa je jamii itajifunzaje kutoka kwake,” aliongeza Celestin.
Wakati huo huo alidai kuwa umoja huo umejipangaa kuhakikisha kuwa unapiga vita mambo mbalimbali kama vile ujinga, umaskini, pamoja na magonjwa kwani hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo wakati mwingine vinasababisha hata majanga mengi kuendelea kutokea katika Bara la Afrika na duniani kwa ujumla.
“Kama viongozi wa dini tutainuka na kisha kupiga vita susla kama hili ni wazi kuwa jamii itafunguka na sisi hapa tuna nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia Serikali zeru katika majanga natoa wito kwa viongozi wa dini kuhakikisha kuwa mnajiwekea tabia ya kusaidia Serikali,” alifafanua zaidi Celestine.
Naye Mwenyekiti wa umoja huo hapa nchini,Mchungaji Philemon Mashauri alisema kuwa pamoja na mikakati mbalimbali ambayo wameiweka ya kusaidia jamii lakini bado wanakabiliwa na changamoto kama vile ukosefu wa ardhi ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali pamoja na ofisi za Umoja huo.
Mashauri aliiomba Serikali kuhakikisha kuwa inayaangalia malengo ya umoja huo na kisha kuwapatia ardhi kwani wana mpango wa kupambana na maradhi ya umaskini na hata majanga mbalimbali ambayo yanaitesa Nchi kwa sasa.

No comments:

Post a Comment