Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Sunday, 7 September 2014
MADAKTARI WATANO WA TANZANIA WAGOMA KWENDA SIERRA LEONE KUTIBU EBOLA
Taarifa zinasema madaktari watano kati ya sita walioombwa na Shirika la Afya Dunia (WHO) kwenda Sierra Leone kutibu Ebola wamegoma.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, daktari pekee aliyekubali kwenda amejulikana kwa jina la Dk. Lyimo.
Madaktari hao walikuwa walipwe kiasi cha Shilingi za Kitanzania milioni 2 kwa siku.
Madaktari wanaodaiwa kukataa kwenda huko ni Dk. Esta Kokugasha Mukasa, Dk. Makame Seif Makame, Dk. Masanja, Dk. Rutabanzibwa na Dk. Ngonyani.
Homa ya Ebola inaelezwa kuua watu zaidi ya 1,900 katika nchi za Afrika Magharibi, wakiwemo madaktari ambao walikuwa wanatoa tiba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment