Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 7 September 2014

MIAKA 30 ILIYOPITA, DOLA ILIUZWA KWA SHS. 17 TU, LEO 1,700!

Ndugu zangu,
Hivi uchumi wetu umeshuka, mfumuko wa bei au ni kuporomoka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania?
Nakumbuka hadi kufikia Agosti mwaka 1984, yaani miaka 30 iliyopita, Dola moja ya Marekani ilikuwa inauzwa kwa Shs. 17 tu, tena wakati huo kilikuwa kipindi cha uchumi wetu kuyumba na tulihitaji sana fedha za kigeni, kwa wanaokumbuka!
Leo hii Dola moja ya Marekani inauzwa Shs. 1,700! Tunaweza kujivuna kama uchumi uko juu au shilingi yetu ina thamani mbele ya fedha za kigeni, hasa Dola? Shilingi yetu leo hii haina thamani mbele ya Shilingi ya Kenya, halafu ile ya Uganda ambayo tulikuwa tumeiacha kwa asilimia kubwa (TShs 1 = UShs 5) leo inatukaribia, achilia mbali fedha za Rwanda na Burundi.
Kwa kuwakumbusha tu ni kwamba, Agosti 1980 Dola ya Marekani iliuzwa kwa Shs. 8 na senti 18; Agosti 1981 Dola ya Marekani iliuzwa kwa Shs. 10 na kiwango hiki kiliendelea hadi mwaka 1983 kabla ya kupanda mwaka 1984 kufikia Shs. 17 na kilibakia hivyo hadi Agosti 1985; Mwaka 1986 Dola iliuzwa kwa Shs. 40; Mwaka 1987 Dola iliuzwa kwa Shs. 65; Mwaka 1988 Dola iliuzwa kwa Shs. 100; Februari 1989 Dola iliuzwa kwa Shs. 124 na senti 9; Agosti 1989 Dola ikapanda hadi Shs. 145; Agosti 1990 Dola ikauzwa kwa Shs. 195; Agosti 1991 Dola ikauzwa kwa Shs. 210; na Agosti 1992 Dola ikapanda hadi Shs. 400!
Ikumbukwe tu kwamba, tangu alipoingia Rais Ali Hassan Mwinyi Oktoba 1985 ndipo Dola ilipopanda hamani na Shilingi yetu ikaporomoka baada ya kuruhusu Soko Huria a.k.a Soko Holela ambalo liliwanufaisha wengi.
Serikali ilipoanza kuchapisha noti za fedha kubwa - Shs. 1,000 (badala ya 100) mpaka kufikia Shs. 10,000 ndipo uchumi ulipoporomoka - au niseme ndipo shilingi ilipoporomoka. Zamani noti kubwa ilikuwa ya Shs. 100 tu!
Tujadili kwa pamoja, nini kilichoporomosha shilingi yetu? Tunajipima vipi katika kukua kwa uchumi ikiwa fedha yetu haina thamani?

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa
0656-331974

No comments:

Post a Comment