
Anaitwa kamanda Samwel Shami. Anagombea nafasi ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA Taifa kupitia Baraza la Vijana (BAVICHA). Huyu jamaa amekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu kwa kipindi kimoja na amefanya mambo makuu yaliyoshangaza wengi katika umri wake mdogo.
Ni kati ya vijana wachache wanaohitajika katika taifa. Amewahi kukamatwa kwa Amri ya Ikulu na akashikiliwa gerezani Kahama kwa kutishia ulaji wa mafisadi katika migodi ya dhahabu ya Barrick Gold akiwa anaongoza harakati za kudai haki za wafanyakazi na wachimbaji wadogo wanaouzunguka mgodi.
Aliandaa petition na kuifikisha Mahakama ya Kimataifa juu ya Social Injustices zinazoendelea ikiwa ni pamoja na mauaji yaliyofanyika miaka ya 1990 wakati migodi inaanza. Amefanya kazi kwa karibu na Tundu Lissu.
Aliwahi kugombea Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki akashika nafasi ya pili kwenye kura za maoni. Amesimamia uchaguzi kama meneja wa kampeni mwaka 2010.
Ni msomi mzuri anayezifahamu siasa za kimataifa ambapo kwa sasa anamalizia shahada ya pili Chuo Kikuu cha ESSEN nchini Ujerumani.
No comments:
Post a Comment