Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameeleza tofauti yake na Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe, akisema imesababishwa na watu aliowaita
wapambe.
Zitto
(37), ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema kuwa hata
kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama kulisababishwa na wapambe hao,
lakini akasisitiza kuwa hana kinyongo tena kwa kuwa alishamwomba Mungu
na sasa amesamehe kabisa.
Tofauti
za wawili hao hazijawahi kutolewa hadharani licha ya mitandao
mbalimbali kuzungumzia kuharibika kwa uhusiano wao ikinukuu habari
kutoka vikao vya ndani vya Chadema.
Hata
hivyo, mapema mwaka huu, Zitto alirushiwa tuhuma nzito na Chadema
kutokana na uhusiano wake na baadhi ya makada wa CCM, lakini mbunge huyo
aliyahusisha maneno hayo na mwenyekiti wake na aliandika maneno makali
dhidi ya Mbowe kwenye ukurasa wake wa facebook.
Lakini
katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika wiki iliyopita nyumbani
kwake Masaki jijini Dar es Salaam, Zitto alionekana kujutia kuharibika
huko kwa uhusiano wao na kusema “wapambe ndiyo wanatugombanisha”.
“Sina
shida yoyote na Mbowe, naamini ipo siku tutagundua wapambe walituathiri
na ndiyo waliotufikisha hapa,” alisisitiza Zitto bila kutaja ni kina
nani hasa.
Zitto alisema
yeye na Mbowe wametoka mbali tangu akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
hafurahii uhusiano wao ukiishia katika hali hiyo.
“Naumia
sana, lakini naamini ipo siku ama nikiwa hai au nimekufa watu wataujua
ukweli,” alisema mwanasiasa huyo kijana aliyepata umaarufu kutokana na
uwezo wake wa kujenga hoja.
Alisema,
akiwa mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu (Daruso) yeye
na mwenyekiti wake ndiyo waliokijenga chama wakati huo Mbowe akiwa
mbunge wa Hai.
Alisema
wakati huo Mbowe alikuwa akienda chumbani kwake kusuka mikakati ya
kuiinua Chadema na kwamba walikuwa wakila chips pamoja na wakati
mwingine kwenye klabu ya usiku ya Bilicanas inayomilikiwa na Mbowe.
Zitto
alisema kuwa wakati huo walikuwa na kampeni yao waliyoiita ‘Real
Madrid’ ambayo ilikuwa na lengo la kuwakusanya
wanasiasa wote wenye ubora na uwezo wa ushawishi kwa umma.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment