Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 September 2014

NYALANDU AKIRI HALI YA UJANGILI NI MBAYA NCHINI


WAKATI juhudi zikifanyika kupambana na ujangili nchini, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema hali ni mbaya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano wa wadau wa maendeleo ya kupambana na ujangili, Nyalandu alisema wanaendelea kubuni mbinu ili kukomesha vitendo hivyo.
Waziri huyo alisema mkutano huo ni mwendelezo wa mkutano uliofnyika Mei mwaka huu ukilenga kuwasilisha uekelezaji wa makubaliano waliyoafikiana kila taifa ili kuona namna gani watasonga mbele katika kukabiliana na viendo vya ujangili.
Kwa upande wa serikali, Nyalandu alisema moja ya hatua walizochukua ni kuajiri askari wanyamapori 430 na hadi Septemba mwaka huu wamelenga kupata askari 900.
Alidai tayari wameanzisha Mamlaka ya wanayamapori iitwayo TAWA ambayo makao makuu yake yatakuwepo mkoani Morogoro na wafanyakazi wote wa Idara ya wanamapori watatakiwa kuhamia huko.
Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa alipongeza hatua hiyo na kudai kuwa inastahili kuungwa mkono kutokana na wao kupiga kelele muda mrefu.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment