Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 September 2014

MWAMALANGA AWAONYA WANATANGAZA NIA

VIONGOZI wa vyama vya siasa wanaotangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 wametakiwa kupima uwezo wao wa kukabiliana na matatizo ya jamii.
Matatizo hayo ni uporaji wa rasilimali, ufisadi, rushwa na mauaji ya albino kabla ya kujitangaza mbele ya wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa Shinyanga Mjini jana na Askofu William Mwamalanga alipofungua Kongamano la Uelewa na Uzalendo kwa vijana 1,400 kutoka vyuo vya madhebu ya dini na kusema viongozi wasio na maadili, uzalendo wenye kiburi na waliokosa usikivu ni chanzo cha mfarakano.
Mchungaji Mwamalanga alisema watu wanaoitaka ikulu mwakani wasitegemee fedha walizo nazo kuwa kigezo cha kuingia huko bali wapime misuli yao endapo inaweza kupambana na kero zinazolitesa taifa.
Shekhe Massoud Amiri Masoud, amekiri kuwa serikali ya awamu ya nne imeshindwa kuwachukulia hatua vigogo wa dawa za kulevya licha ya kupewa orodha ya majina yao mwaka 2006 lakini hakuna aliyekamatwa.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment