WANAFUNZI 21,540 watafanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mkoani Iringa mwaka huu ikiwa ni pungufu ya waliofanya mtihani huo mwaka jana.
Mwaka jana wanafunzi 23,149 mkoani hapa walifanya mtihani huo ambao mwaka huu utaanza kesho Septemba 10 hadi 11 nchini kote.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Iringa, Joseph Mnyikambi alisema wanafunzi wa shule 458 kati ya 484 ndio watakaofanya mtihani huo.
Alisema kati ya wanafunzi watakaomaliza elimu ya msingi mwaka huu wavulana ni 9,779 na wasichana 11,761 ukilinganisha na mwaka jana ambapo wavulana walikuwa 10,753 na wasichana 12,396 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi.
Alisema kuwa maandalizi yamekamilika ambapo vifaa vimepelekwa katika halmashauri zote za mkoa huo.
CREDIT: TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment