Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday, 13 September 2014
MILIONI 24 ZACHANGWA KUJENGWA BWENI LA WATOTO WA KIKE
Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog
ARUSHA: ZAIDI ya Milioni 24 zimechangwa na wadau mbalimbali wa elimu mkoani Arusha kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Lonange.
Akiongea jana mara baada ya kuchangishwa kwa fedha hizo
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Goodlucky ole Medeye alisema ujenzi wa bweni hilo utaweza kuwasaidia watoto wa kike
Medeye alidai kuwa asilimia kubwa ya watoto wa kike ambao wa wanapata matatizo mbalimbali likiwemo tatizo la mimba za utotoni ni kutokana na ukosefu wa mabwani ambapo watoto hao hukumbwa na vishawishi pindi wanapotoka au kurudi majumbani
“Nasema kuwa bado jamii inahitajika kujua kuwa watoto wa kike wanapaswa kuwa na mabweni na wakiwa na mabweni sio raisi sana kukumbana na kinachotokea hivyo tuache tabia ya kukwepa kusaidia watoto wakike au elimu hususani mabweni”aliongeza Medeye
Kutokana na hilo alisema kuwa kwa sasa ana mikakati mbalimbali ya kuweza kujenga na kuhamaisha ujenzi wa mabweni katika jimbo lake ambalo lina idadi ya watoto wa kike wengi sana na hivyo jamii nayo inatakiwa kumuunga mkono ili kuwasaidia watoto hao.
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo ya Lonange Dkt Prisilla Kambaine alisema kuwa tayari mpaka sasa wameshaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia watoto wa kike waishio pembezoni mwa shule hiyo lakini na mikoa mingine kwa kuhakikisha kuwa wanajenga mabweni
Dkt Prisilla alisema kuwa endapo kama wataweza kupata mabweni ya uhakika basi watawaokoa watoto wa kike dhidi ya majanga mbalimbali yakiwemo ya ufaulu hafifu na hivyo ufaulu utaongezeka sana katika Nchi ya Tanzania.
Alimalizia kwa kusema kuwa nao wazazi wanatakiwa kuhamasisha ujenzi wa mabweni kwani pia kama wamiliki wa shule mbalimbali watakuwa na hamasa ya kujenga mabweni lakini kwa uapande wa wawazazi hawana hamasa hiyo itakuwa ni kazi bure kabisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment