Wananchi wakisaidia kuokoa vitu katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni baada ya moto kuzuka jana kabla ya swala ya adhuhuri.
Haya ni mabweni ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mivumoni yaliyoko kwenye eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam ambayo yaliungua moto katika tukio la mwezi uliopita.
NA ROMANA MALLYA
Mwezi mmoja tu baada ya msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam kuungua, moto mwingine umezuka jana muda mfupi kabla ya swala ya adhuhuri na kuteketeza chumba cha wanafunzi.
Haya ni mabweni ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mivumoni yaliyoko kwenye eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam ambayo yaliungua moto katika tukio la mwezi uliopita.
NA ROMANA MALLYA
Mwezi mmoja tu baada ya msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam kuungua, moto mwingine umezuka jana muda mfupi kabla ya swala ya adhuhuri na kuteketeza chumba cha wanafunzi.
Awali, moto huo uliteketeza vitu vyote vilivyokuwa kwenye ghorofa ya juu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, akizungumza jana na NIPASHE eneo la msikiti huo, alisema tukio hilo lilitokea saa 6: 00 mchana ghorofa ya kwanza.
Alisema moto huo umeteketeza chumba hicho ambacho wanafunzi walikuwa wakikitumia kama ‘kempu’ ya kujisomea kujiandaa na mitihani.
Alisema moto huo umeteketeza magorodo manne na mali mbalimbali za wanafunzi hao pamoja na madaftari yao.
Alisema chumba hicho ambacho awali kilikuwa ni darasa, kwa sasa wanafunzi walikuwa wanakitumia kwa kulala na kujisomea.
Alisema chanzo cha moto huo haki jafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea sambamba na ule wa awali ambao haujakamilika.
“Tutakapokamilisha uchunguzi wote ndiyo tutaweza kueleza nini kifanyike, ila kwa sasa tunawaomba waumini na wakazi wa maeneo haya wawe watulivu ili timu hii inayoendelea na uchunguzi ikamilishe kazi yake,” alisema.
Katibu wa Msikiti huo, Sheikh Abdallah Mohamed, alisema kuwa kulikuwa na fundi ambaye alikuwa akitengeneza umeme.
“Ghafla tuliona moshi umetanda kwenye eneo hili, cha ajabu fundi ambaye alikuwa akitengeneza hajaonekana tena baada ya tukio hili na tunamtafuta,” alisema na kuongeza:
“Tunashangaa kwa nini matukio haya ya moto yanatokea wakati kukiwa na mkusanyiko wa waumini wanaotaka kuswali, tutachunguza chanzo ni nini,” alisema.
Mwezi uliopita, moto ulitokea msikitini hapo majira ya jioni kwenye ghorofa ya tatu na kuteketeza mali zilizokuwamo na kudaiwa kusababisha hasara ya Sh. milioni 500.
Sehemu hiyo iliyoteketea ilikuwa ikitumika kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Mivumoni.
CHANZO: NIPASHE


No comments:
Post a Comment