Naibu Waziri
wa Fedha, Mwigulu Nchemba
Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog
ARUSHA: NAIBU Waziri
wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameitaka
mifuko ya hifadhi ya jamii kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha
mahakamani waajiri ambao wamekuwa hawawasilishi michango ya
wanachama wao
hali ambayo imekuwa ikichangia kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara.
hali ambayo imekuwa ikichangia kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara.
Aliyasema
hayo wakati akifungua mkutano wa 24
wa wanachama wa hifadhi ya mfuko wa jamii wa PPF unaoendelea mjini hapa.
Alisema
kuwa, hali hiyo imekuwa ikichangia umaskini mkubwa kwa kuwa wapo baadhi za wanachama
ambao wanakosa haki zao za msingi kutokana na makato yao kubaki kwa waajiri kwa
kipindi cha miaka mingi tofauti na sheria ya mifuko inavyosema.
Nchemba aliongeza kuwa, kitendo cha
mifuko ya jamii kuendelea kulalamikia hali hiyo ya waajiri
kutowasilisha michango hiyo, bado haitoshi ila kinachotakiwa kuanzia sasa ni
kuwachukulia hatua ili kukomesha tabia hiyo ya kuwanyanyasa baadhi ya
wafanyakazi.
"Kila ninapokwenda
kwenye mikutano ya mifuko ya hifadhi ya jamii nimekuwa nikikutana na changamoto
hiyo ambayo ni kilio cha mifuko yote nchini, sasa umefika wakati kuangalia sheria
zinasemaje kwani wanaoteseka ni Watanzania wenzetu," alisema .
Alifafanua
zaidi kuwa, kuanzia sasa wizara ya fedha imeweka mikakati mbalimbali ya
kuhakikisha kuwa inawafuatilia baadhi ya waaajiri wanaowanyima wafanyakazi haki
zao za msingi na kuhakikisha kuwa wote wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo
kufikishwa mahakamani.
Aidha aliitaka
mifuko hiyo kuwasilisha taarifa ya mapato na matumizi kila mwaka ili kuwezesha
wanachama wake kuwa na imani na chombo chao
na hivyo kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikichangiwa kutokana na
kutokuwepo kwa taarifa hizo kwa wakati.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF) Ramadhan Kijja ,alisema kuwa, mfuko huo umeanzisha utaratibu wa kusomesha
watoto wa wanachama wao toka elimu ya awali hadi kidato cha sita ikiwa ni njia
mojawapo ya kuendeleza wasomi wanaonufaika na mfuko huo.
Alisema
kuwa, hadi sasa hivi wametumia kiasi cha
shs 750 milioni ambazo zimewanufaisha wanafunzi elfu moja mia moja ambao
wanapata elimu kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita ambapo hali hiyo
imewaondolea mzigo wanachama wake hususani wale
waliokuwa hawana uwezo.
Alifafanua
kuwa,mbali na kuwasaidia wanafunzi hao pia thamani ya mfuko wa PPF umeongezeka kutoka trilioni 1.09 kwa mwaka 2012 hadi kufikia trilioni 1.48 kwa
mwaka 2013 sawa na ongezeko la asilimia 36.27.
No comments:
Post a Comment