Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 10 March 2014

TAARIFA YA OFISI YA LOWASSA KUHUSU 'NOTI YA FEDHA' YENYE SURA YAKE

Noti ya shilingi mia tano iliyochorwa sura ya Edward Lowassa


Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mhe. Edward Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.

Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo hicho siyo 
utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi.

Mhe. Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa (MB)

SOURCE: WANABIDII

No comments:

Post a Comment