Kikaragosi hiki nimekitoa hapa: lukemusicfactory.blogspot.com
Na Daniel Mbega
HISTORIA inaonekana kuwa chungu kwa mabigwa wa soka
Tanzania Bara, Yanga, dhidi ya timu za Misri baada ya kuondolewa kwenye
mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia matokeo ya jumla kuwa 1-1.
Awali Yanga ilishinda kwa bao 1-0 jijini Dar es
Salaam, na katika mchezo wa jana uliofanyika mjini Alexandria, Al Ahly
ikashinda bao 1-0 katika dakika 90 kabla ya sheria ya mikwaju ya penalty kutumia,
ambapo mabingwa hao wa Afrika wakafanikiwa kupenda.
Mechi ya jana ilikuwa ya 14 dhidi ya timu za Misri
kwa Yanga, ambapo timu hiyo ya Tanzania imefanikiwa kushinda mechi moja tu,
kutoka sare tano na kufungwa mechi 8, huku ikifunga mabao 8 na kupachikwa 29.
Hata hivyo, hiyo ilikuwa mechi ya 8 kuzikutanisha
Yanga na Al Ahly, ambapo Yanga ilishinda mara moja tu katika mchezo uliofanyika
jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, ikitoka sare mara mbili tu na
kupoteza mechi tano.
Kwa bahati nzuri au mbaya, timu hiyo ya Jangwani
imepambana na timu tatu tu za Misri katika historia yake – ikiwa imecheza na Al
Ahly mara nane na kufungwa mechi tano, huku ikilazimisha sare mara mbili nyumbani.
Lakini kwa jumla ya mechi zote hizo nne (nne zikiwa katika Klabu Bingwa na
mbili za Kombe la Shirikisho), imefungwa mabao 19-5!
Imewahi kucheza na Ismaily kwenye Klabu Bingwa
Afrika mwaka 1992, lakini ikafungwa nyumbani 2-0 na kulazimisha sare ya 1-1
mjini Ismailia.
Mwaka 2000 Yanga ilifungwa mabao 4-0 kule Cairo na
Zamalek baada ya kuwa imelazimisha sare ya 1-1 mjini Dar es Salaam katika Kombe
la Washindi, na mwaka 2012 ikalazimisha pia sare ya 1-1 mjini Dar es Salaam
dhidi ya Zamalek kabla ya kuchapwa bao 1-0 jijini Cairo kwenye Ligi ya Mabingwa
Afrika.
Rekodi ya Yanga katika michezo ya kimataifa
hairidhishi wala kufurahisha, inakera na inakinaisha kuizungumzia. Ni mara tatu
tu katika historia yake imewahi kufanya vizuri – mwaka 1969 ilipotolewa na
Asante Kotoko kwa shilingi, na mwaka 1970 ilipofungwa 2-0 na Kotoko kwenye
Uwanja Huru mjini Addis Ababa baada ya kutoka sare mechi zote mbili. Mara zote
mbili timu hiyo ilitolewa kwenye robo fainali.
Mara ya tatu ilikuwa mwaka 1998 wakati kikosi
kilichoundwa na akina Edibily Lunyamila kilipofanikiwa kufuzu katika hatua ya
makundi (robo fainali) ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ukiacha kiwewe cha kuvurunda kwenye mechi za
kimataifa, Yanga kwa ujumla haina ubavu mbele ya timu kutoka Afrika ya
Kaskazini. Haina kabisa na siyo suala la ushabiki wala kukosa uzalendo.
Iwe kwenye michuano ya Afrika ama ile ya Afrika
Mashariki na Kati, timu hiyo daima huwa haitambi mbele ya timu kutoka Sudan,
Misri, Tunisia, Libya au Morocco ambazo imewahi kukumbana nazo.
Kati ya mechi 30 ilizocheza na timu kutoka ukanda
huo, Yanga imeshinda mechi mbili tu, ikilazimisha sare 13 na kufungwa 15! Katika
mechi zote hizo imefunga mabao 21 tu huku ikibugizwa mabao 53.
Mechi za Yanga na timu za Misri:
P W D L
GF GA
14 1 5 8
8 29
Yanga na timu za Afrika Kaskazini:
P W D L
GF GA
30 2 13 15
21 53
Rekodi ya Yanga katika michuano ya kimataifa dhidi
ya timu kutoka Afrika Kaskazini, ikiwemo Sudan:
Klabu Bingwa Afrika:
1973
Raundi ya Kwanza
Yanga 1-2 Al-Merreikh (Sudan)
Al-Merreikh 1-1 Yanga
1982
Raundi ya Pili
Al-Ahly (Misri) 5-0 Yanga
Yanga 1-1 Al-Ahly
1988
Raundi ya Kwanza
Yanga 0-0 Al-Ahly (Misri)
Al Ahly 4-0 Yanga
1992
Raundi ya Kwanza
Yanga 0-2 Ismaili (Misri)
Ismaili 1-1 Yanga
1998:
Robo Fainali (Nane Bora)
Kundi B
Raja Casablanca (Morocco) 6-0 Yanga
Yanga 3-3 Raja Casablanca
2007
Raundi ya 16 Bora
Espérance (Tunisia) 3-0 Yanga
Yanga 0-0 Esperance
2009
Raundi ya Pili
Al-Ahly (Misri) 3-0 Yanga
Yanga 0-1 Al Ahly
2012
Raundi ya Pili
Yanga 1-1 Zamalek
Zamalek 1-0 Yanga
2014
Yanga 1-0 Al Ahly
Al Ahly 1-0 Yanga
*penalty Al Ahly 4-3 Yanga
Kombe la Shirikisho
2007
Raundi ya Kati
Yanga 0-0 Al Merreikh (Sudan)
Al Merreikh 2-0 Yanga
2008
Raundi ya Pili
Al-Akhdar (Libya) 1-0 Yanga
Yanga 0-1 Al Akhdar
Kombe la Washindi
2000
Yanga 1-1 Zamalek (Misri)
Zamalek 4-0 Yanga
MICHUANO YA CECAFA
1986
Fainali
Al Merreikh 2-2 Yanga [aet, 4-2 pen]
1988
El Hilal 2-0 Yanga
1994
El Hilal 1-1 Yanga
1995
Mourada 1-1 Yanga
1999
Al Hilal 1-2 Yanga
Khartoum3 0-0 Yanga
No comments:
Post a Comment