Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 11 March 2014

MCHUNGAJI ANAYEHUBIRI AKIWA NA NYOKA AFARIKI DUNIA BAADA YA NYOKA HUYO KUMNG'ATA

Pasta anayejulikana kuhubiri akiwa amemweka nyoka shingoni ameaga dunia. Pasta Jamie Coots anayeamini kuwa kinga hutoka kwa mungu aliweza kupoteza maisha yake baada nyoka huyo wa sumu kumuuma akiwa akihubiria mbele ya maumini.

Ilikuwaje hadi pasta huyo kuhubiri na nyoka mgongoni?

Kupitia andiko la Marko 16:15-18, pasta huyo anaamini kuwa Yesu aliweza kuwaambia wakristo wote kuwa wanaweza kushika nyoka na hatawaumiza wala kuwadhuru bora tu uwe umebarikiwa na mungu mwenyewe.

Pasta huyo wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus Name aliumwa na nyoka huyo mbele ya kanisa lake na ilimbidi kukimbizwa hadi nyumbani kwake bila kupelekwa hospitalini.

Wauguzi walipowasili nyumbani kwake waliweza kufukuzwa huku pasta huyo akiwa na imani kuwa mungu atamtibu ugonjwa wake, jambo ambalo halikufanyika.

Chanzo: Udaku Specially

No comments:

Post a Comment